Jokate Mwegelo Azindua Kidoti Club
Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 Jokate Mwegelo, siku ya leo amezindua rasmi Club yake ambayo inaitwa Kidoti Club itakayokuwa ikihusika na maswala ya urembo. Mrembo huyo pia amezindua mitindo mipya ya nywele, ambayo inajuliakana kama Kidoti Brand.
Katika club hiyo ya Kidoti itakua ikijihusisha na maswala ya kutoa ushauri katika jamii ikiwa pamoja na taarifa za kimuziki, filamu na kazi za kisanaa kiujumla kwa kila rika katika jamii, Kidoti Club lengo lake kubwa haswa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na kuwapa nafasi watu wengine waweze kujiunga.
Kiongozi wa club hiyo Miss Mwegelo ambaye ni Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006,amesema kuwa ili uweze kupata nafasi ya kujiunga na kuwa mwanachama katika clabu hiyo, unatakiwa kutuma neno kidoti kwenda namba 15678, baada ya hapo utaanza kupata taarifa mbali mbali kuhusiana na Kidoti Club.
CREDIT:GONGAMIX
No comments:
Post a Comment