Wednesday, December 4, 2013

PENZI LA SUGAR MOMMY LA SABABISHA KIFO CHA KIJANA NI BAADA YA KUMWAGWA NA KUFIKIRIA JINSI ATAKAVYOYAMISI MALAVIDAVE

Michael Jaja ni kijana mwenye umri usiozidi miaka 22 ni mkazi wa kitongoji kimoja kilichojulikana kwa jina la Tema huko nchini Ghana. Michael alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama mtu mzima mwenye umri wa miaka 48, mama huyo aliekuwa ana dhamini matumizi ya maisha ya raha ya kinda hilo kwa kipindi chote walicho kuwa pamoja na kudiriki kumsogeza ndani ya mjengo wake wa dhamani na kumpatia usafiri kwa ajili ya kurahisisha maisha ya mizunguko ya kila siku ndani ya kitongoji cha Tema. Kipindi hicho chote kijana alilewa na maisha ya raha na kujua kuwa maisha ndiyo haya akuna mwingine kama yeye. kwani mama aliweza kudhamini kila kitu ikiwa na safari za Umangani  na Uchina kama vacation na shopping za pamba nyepesi kwa kinda huyo. Sasa basi mambo yalikuja kubadirika na kugeuka simanzi baada ya mfadhili mkubwa wa raha hizo kuingia mjini akitokea ng'ambo alikokuwa akipiga box na kutuma pesa kwa jimama  ilikujikimu kimaisha pamoja na kujenga nyumba ya kifahari na kununua usafiri wa hapa na pale. Sasa mjeda huyo alivyo karibia kutimba tu mama akamwambia kijana anaitaji kumpisha mzee mzima na yeye ashike hamsini zake hakuna kupika wala kupakuwa achukua kilicho chake na aishie. Kijana kusikia vile alipatwa na mawazo na kukosa raha kabisa kwani alizoea raha za shopping , usafiri na trip za Umangani hakakosa amani kabisa baada ya kufikiria yote hayo sasa yata bakia kumbukumbu. Ndipo alivyo chukua uamuzi wa kujinyonga kwani asinge weza kuishi bila sugar mommy na zaidi ya yote raha zote angezisikia kwenye nyozi  tu. Vijana tusipende vya kunyonga tujipinde kiroho safi kufugwa siyo issue mfadhili akichoka yasije kukuta ya kijana Michael.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake