Maustadh wakisoma dua kwenye hitma ya mama yake na Latifa. Hitma hiyo ilifanyika Brooklyn NY. Watanzania kutoka sehemu mbalimbali walihudhuria hitma hiyo. Mama yake Latifa Mahundi na pia ni bibi mzaa mama wa Bahia na Ashraf.
Ustadh Mafutah mwenyekiti wa CCM tawi la New York akiwa na mkuu wa wilaya ya Springfield bwana Kibodya, Bwana Kibodya alikuwepo nae katika hitma hiyo. Bwana kibodya aliongozana na watu wengine kutoka Springfield ili kuongeza umoja na upendo katika shughuli hiyo.
Ustadh kutoka Yemen akisoma dua kwenye hitma hiyo kama unavyoona kwenye picha
DMK pamoja na AJ Ubao kutoka DC walihudhuria pia kwenye hitma hiyo kama unavyowaona kwenye ukodak.
DMK ni Promoter maarufu sana kwa Marekani na moja ya kazi yake ni kuhakikisha Watanzania wanakutana iwe kwenye starehe au kwenye shughuli za misiba. Kwahiyo kuwa kwake hapa unaweza kugundua kuwa siyo wakati wa starehe tu hata kwenye shida yupo mstari wa mbele.
2 comments:
mashallah imefana hitma si haba mashallah Allah amlaze mahali pema peponi na pamoja na sisi tuliopo njiani katika safari hiyo na wakina mama wamependeza kwa sare zao mashallah mashallah
aj ubao ungekuwa ustadha bwana umependeza na umetulia tuli dua inapanda mashallah aj ubao
mummy aj ubao nayeye jamani tungemuona mbona picha kwa akina mama hatujapata kuwaona vizuri jamani
aj ungetiye kazu yako ya ki sheikh ungetoka mwangau ile mbayaaa
Post a Comment