Pichani ni ndege ambayo yaiendeshwi na binadamu maarufu kama Drones ( Unamanned aerial Vehicles) ambayo ni kati ya mbili zilizozinduliwa rasmi siku ya jumanne tayari kwa matumizi ya shughuli za ulinzi katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Anaonekena pia Mkuu wa Idara ya Operesheni ya Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa ( DPKO) Bw. Herve Ladsous (katikati) akipewa maelezo kuhusiana na kifaa hicho. ( picha kwa hisani ya UN)
Na Mwandishi
Maalum
Umoja wa Mataifa
jana disemba tatu
umetimiza azma yake ya
kutumia teknolojia za kisasa katika
operesheni zake za ulinzi wa amani baada ya kuzindua rasmi matumizi ya ndege maalumu ambao haziendeshwi
na binadamu maarufu kama Drones au kwa
jina la kitaalam ‘unamanned aeria vehichles ( UAVs).
Kwa mujibu wa
taarifa kutoka Umoja wa Mataifa, uzinduzi
wa zana hizo umefanyika huko Goma
ambako ni makao makuu ya Jimbo la Kivu
ya Magharibi katika DRC na kushuhudiwa
na watu wa kada mbalimbali wakiwamo baadhi ya viongozi wa juu wa Umoja
wa Mataifa, serikali na waandishi wa
habari.
Akinukuliwa wakati wa uzinduzi wa UAVs ambazo lengo lake ni
kukusanya taarifa za kiitelejesia zitakazo saidia kutambua mapema
hali ya hatari inayowakabili wananchi wa
maeneo hayo na kutoa ulinzi na vile vile kubaini mienendo ya makundi ya
wanagambo wenye silaha . Kiongozi mkuu wa
Idara ya Operesheni za Kulinda
amani za Umoja wa Mataifa ( DPKO) Bw.
Herve Ladsous alikuwa na haya ya kusema
“ Hii ni mara
ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa ya matumizi ya teknolojia
hizi za hali ya juu katika
operesheni za ulinzi wa amani”.
Na Kuongeza “Umoja wa Mataifa
unahitaji kutumia aina ya zana hizi ili kutekeleza vema mamlaka zake”
Eneo la Mashariki ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa muda mrefu limekuwa likikabiliwa na mapigano kati ya Mejeshi ya Serikali ya Kongo na makundi
mbalimbali ya wanagambo wenye silaha
likiwamo kundi maarufu la M23 linaloundwa na wanajeshi walioasi kutoka Jeshi
la kitaita la DRC ( FARDC).
Kuzinduliwa kwa
matumizi ya teknolojia hizo za kisasa, kunafuatia uamuzi wa Baraza Kuu
la Usalama la Umoja wa Mataifa hasa kwa kuzingatia ugumu na ukubwa wa eneo
ambalo liko chini ya mamlaka ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kupitia MONUSCO
Mkuu wa DPKO Bw. Ladsous amefafanua zaidi kwa
kusema kwa kuanzia ni drones mbili ambazo zitaanza kufanya
kazi lengo likiwa ni kuwa na zana zaidi ya hizo kwa matumizi ya muda wote na
kufanya kazi katika eneo kubwa.
Akifafanua zaidi
Bw. Herve Ladsous amesema kwamba
matumizi ya zana hizo umejidhirisha zaidi hususani katika siku za hizi karibuni ambao
kundi la M23 limeanza
kusambaratika kwa kile alichosema huenda kundi hilo limebaini kwamba kuna mabadiliko
makubwa katika eneo hilo la Mashariki ya
DRC hata kabla ya kuanza rasmi kwa matumizi ya
zana hizo.
Naye Kamanda
Mkuu wa MONUSCO Jenerali Santos Cruz yeyé amesema uwepo kwa aina hiyo ya
teknolojia kutawawezesha kuchanganya taarifa zitakazokusanywa na zana hizo pamoja na zile zitakazo kusanywa na wataalamu walioko ardhini
Na kuongeza “
tutaweza kuchunguza mienendo ya makundi ya wanamgambo wenye silaha, na mienendo ya wananchi, tutaweza pia kuona
silaha ambao zinabebwa na wananchi walioko ardhini, ni rahisi pia hata kuwaona
watu walioko katikati ya misitu mikubwa, picha ambazo zinaweza kupatika hata katika
umbali wa kilometa tatu”
No comments:
Post a Comment