Tuesday, December 3, 2013

UMOJA WA MATAIFA WAZINDUA RASMI MATUMIZI YA DRONES DRC

Pichani ni ndege ambayo yaiendeshwi na binadamu maarufu kama Drones ( Unamanned aerial Vehicles) ambayo ni kati ya mbili zilizozinduliwa rasmi siku ya jumanne tayari kwa matumizi ya shughuli za ulinzi katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Anaonekena pia Mkuu wa Idara ya Operesheni ya Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa ( DPKO) Bw. Herve Ladsous (katikati) akipewa maelezo kuhusiana na kifaa hicho. ( picha kwa hisani ya UN)

Na  Mwandishi Maalum
Umoja wa Mataifa  jana  disemba   tatu     umetimiza azma yake  ya kutumia  teknolojia za kisasa katika operesheni zake za  ulinzi  wa amani baada ya  kuzindua rasmi  matumizi ya ndege maalumu ambao haziendeshwi na binadamu  maarufu kama  Drones au kwa   jina la kitaalam ‘unamanned aeria vehichles ( UAVs).
Kwa  mujibu wa taarifa  kutoka  Umoja wa Mataifa,  uzinduzi  wa zana  hizo umefanyika huko Goma ambako ni  makao makuu ya Jimbo la Kivu ya Magharibi katika  DRC na  kushuhudiwa  na watu wa kada mbalimbali wakiwamo baadhi ya viongozi wa juu wa Umoja wa Mataifa,  serikali na waandishi wa habari.
Akinukuliwa wakati wa uzinduzi wa  UAVs ambazo lengo lake  ni  kukusanya taarifa za kiitelejesia zitakazo saidia kutambua mapema hali  ya hatari inayowakabili wananchi wa maeneo hayo  na kutoa ulinzi  na  vile vile kubaini mienendo ya makundi ya wanagambo wenye silaha . Kiongozi mkuu wa  Idara ya Operesheni za  Kulinda amani  za Umoja wa Mataifa ( DPKO) Bw. Herve Ladsous alikuwa na haya ya kusema
“ Hii ni mara  ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa ya matumizi ya  teknolojia  hizi za hali ya juu katika  operesheni za ulinzi wa amani”.  Na Kuongeza  “Umoja wa Mataifa unahitaji kutumia aina ya zana hizi ili kutekeleza vema mamlaka zake”

Eneo la Mashariki ya  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa muda mrefu  limekuwa likikabiliwa na  mapigano kati ya  Mejeshi ya Serikali ya Kongo na makundi mbalimbali ya wanagambo wenye silaha  likiwamo kundi maarufu la M23 linaloundwa na wanajeshi walioasi kutoka Jeshi la kitaita la DRC ( FARDC).
Kuzinduliwa kwa  matumizi ya teknolojia hizo za kisasa, kunafuatia uamuzi wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa hasa kwa kuzingatia ugumu na ukubwa wa eneo ambalo  liko chini ya  mamlaka ya  walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa   kupitia MONUSCO
Mkuu wa DPKO Bw. Ladsous amefafanua zaidi kwa kusema  kwa kuanzia ni    drones mbili ambazo zitaanza kufanya kazi  lengo likiwa ni  kuwa na zana  zaidi ya hizo kwa matumizi ya muda wote na kufanya kazi  katika eneo kubwa.
Akifafanua zaidi   Bw. Herve Ladsous amesema kwamba  matumizi ya   zana hizo  umejidhirisha zaidi hususani  katika siku za hizi karibuni  ambao   kundi la M23  limeanza kusambaratika  kwa kile alichosema  huenda kundi hilo limebaini kwamba kuna mabadiliko makubwa  katika eneo hilo la Mashariki ya DRC hata kabla ya kuanza rasmi kwa matumizi ya  zana hizo.
Naye  Kamanda Mkuu wa MONUSCO Jenerali Santos Cruz yeyé amesema uwepo kwa aina hiyo ya teknolojia  kutawawezesha  kuchanganya taarifa zitakazokusanywa na  zana hizo pamoja na zile  zitakazo kusanywa  na wataalamu walioko ardhini
 Na kuongeza “ tutaweza kuchunguza mienendo ya makundi ya wanamgambo wenye silaha,   na mienendo ya wananchi, tutaweza pia kuona silaha ambao zinabebwa na wananchi walioko ardhini, ni rahisi pia hata kuwaona watu walioko katikati ya misitu mikubwa, picha ambazo zinaweza kupatika  hata katika  umbali wa kilometa tatu”

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake