Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa, David Msuya akiwa Hopitali
Hali ya Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa, David Msuya aliyelazwa kwenye Taasisi ya Moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), inaendelea kutengamaa.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa taasisi hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji, alisema Mzee Msuya anaendelea vizuri na kwamba alikuwa akitarajiwa kuruhusiwa kurudi nyumbani wakati wowote jana.
“Mzee wetu anaendelea vizuri na hali yake imetengamaa na wakati wowote leo (jana) ataruhusiwa kurudi nyumbani,” alisema.
Kuhusu hali ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi na Utumishi), Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Haroun Ali Suleiman Meneja huyo alisema hali ya waziri huyo nayo inaendelea vizuri.
Wakati huohuo, Mbunge wa Chalinze Said Bwanamdogo amelazwa kwenye Taasisi ya Magonjwa ya Mifupa na Fahamu (MOI), kwenye Kitengo kinachohitaji uangalizi maalumu (ICU) cha hospitali hiyo.
Kwa mujibu wa Meneja wa Ustawi wa Jamii na Mawasiliano wa Moi, Jumaa Almasi, hali ya Bwanamdogo aliyepokelewa hospitalini hapo siku ya Jumanne inaendelea vizuri tofauti na siku aliyopokelewa, ingawa hata hivyo hakuwa tayari kueleza ugonjwa unaomsumbua.
Almasi alisema kuwa Juzi jioni Rais Jakaya Kikwete pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete walifika hospitalini hapo kumjulia hali mbunge huyo.
Aidha, alisema majeruhi wa tukio la ujambazi lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita huko Newala mkoani Mtwara Isaya Mwagala na kusababisha vifo vya askari polisi wawili na raia mmoja, amefikishwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa Almasi, majeruhi huyo alipokelewa juzi usiku saa mbili Moi, na baadae kuhamishiwa MNH.
Juhudi za kumtafuta Afisa Habari wa MNH, Aminieli Eligaesha hazikuzaa matunda kwa kile kilichoelezwa yupo kwenye kikao cha utawala nje ya hospitali hiyo na hata pale NIPASHE ilipomtafuta kwa njia ya simu, simu yake ya mkononi iliita bila ya kupokelewa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake