Tuesday, January 14, 2014

LOWASSA : BODA BODA NI MUHIMU


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, anatarajia kukutana na Kamati Kuu ya shirikisho la bodaboda Saccos kwa ajili ya ufunguzi wa Saccos hiyo.
Ufunguzi huo unatarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam, lengo likiwa ni pamoja na kuwakwamua kiuchumi madereva bodaboda nchini.

Ofisa habari wa Chama cha bodaboda mkoa wa Ilala, Abdallah Bakari, alimshukuru Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), kwa kutambua umuhimu na uwepo wa bodaboda na kwamba ni mfano wa kuigwa na viongozi wengine.

Bakari amewataka viongozi wengine kuiga mfano huo na kuwasaidia vijana ili kuwawezesha kuinua vipato vyao na kuwawezesha pia kimiliki pikipiki na kuondoa matatizo yanayojitokeza.

Pia, ameziomba asasi na watu mbalimbali kuwasaidia madereva bodaboda walioko hospitalini kutokana na ajali, kupata matibabu ili waweze kurejea kazini kwani wamekuwa wakikaa kwa kipindi kirefu bila kupatiwa matibabu na wengine kufariki.
Madereva hao pia wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za barabara ili kupunguza ajali.

2 comments:

  1. Lowassa ni mnafiki na kila kitu kwake ni siasa. Badala ya kuweka usalama wa raia mbele, yeye anafikiria urais matokeo yake anato matokea yake anawapotosha wadanganyika

    ReplyDelete
  2. Sasa hivi tunalia na ajali za bodaboda kugongana, kugongwa na magari.Lakini miaka ijayo tutalia watoto wetu(wadogo) kugongwa na hizi boda boda.Hawa jamaa hawako makini barabarani hata kidogo

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake