Johannes Franciscus 'Hans' van der Pluijm
Wakati kocha mpya wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Yanga ya jijini Dar es Salaam, Johannes Franciscus ‘Hans’ van der Pluijm, anatarajiwa kuondoka nchini leo kuifuata timu hiyo nchini Uturuki, imefahamika kuwa atakuwa mshauri wa ufundi katika kikosi hicho.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jijini jana kutoka kwa chanzo chetu, zilieleza Mholanzi huyo ataingia mkataba wa miezi sita na atakuwa ni mshauri wa ufundi wa timu hiyo.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kwamba endapo uongozi utaridhishwa na kiwango cha kocha huyo mara baada ya kumalizika msimu huu wa 2013/ 14 ndio atapewa mkataba mrefu.
"Sasa hivi tuko katika maandalizi ya kocha kuondoka kwenda Uturuki kuungana na timu na suala la mkataba atasaini mkataba mfupi wa kumalizia msimu halafu baadaye ndiyo tutajua kama ataendelea na sisi au la kutokana na matunda ya kazi yake yatakayoonekana," kilisema chanzo chetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Abdallah Bin Kleb, hakupatikana jana kuzungumzia mchakato huo wa kupata kocha ulivyofikia.
Kocha huyo ambaye aliwahi kuiongoza klabu ya Berekum Chelsea ya Ligi Kuu ya Ghana anatajwa kuwa ni kocha anayependa kuona wachezaji wanajituma wakati wote.
Kibarua kikubwa cha kocha huyo mpya ni kuifanya Yanga ipate matokeo mazuri katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika ambayo itaanza napema mwezi ujao.
‘Hans’ van der Pluijm aliyezaliwa Januari 3, 1949 alitua Afrika kwa mara ya kwanza 999 alipojiunga na Ashanti Gold ya Ghana na baadaye alihamia Saint George SA ya Ethiopia na 2010 alitua B-juniors Feyenoord ya Ghana ambayo ni tawi la timu hiyo ya Rotterdam.
MKWASA ASIFIA MAZOEZI
Akizungumza juzi katika mahojiano na kituo kimoja cha redio cha hapa nchini, Mkwasa alisema kikosi chake kinaendelea vyema na mazoezi na lengo lao la kuweka kambi Uturiki litazaa mafanikio.
Mkwasa alisema wachezaji wanapata muda mrefu wa kufanya mazoezi na muda wote wakiwa huko wanazungumza lugha moja ya soka na si mazungumzo mengine.
Kocha huyo aliyejiunga Yanga akitokea Ruvu Shooting ya mkoani Pwani alisema, pia amefurahishwa na kiwango cha timu yake kilichoonyeshwa kwenye mechi ya kwanza dhidi ya timu ya Ankara Sekerspor inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Uturuki ambayo licha ya kupata ushindi wa mabao 3-0 lakini iliwapa changamoto na ushindani.
"Tumepata mazoezi mazuri na yenye faida kwetu, kwa kweli tutarejea nchini tukiwa tumebadilika," alisema kocha huyo.
Alieleza kuwa hali ya hewa si ya baridi sana kama walivyotarajia kuikuta na inawapa nafasi nzuri wachezaji kujifua.
Alisema pia bado hawajajua watacheza lini mechi ya pili ya kirafiki lakini akathibitisha kwamba wenyeji wao wanaendelea kuwatafutia timu.
"Nadhani itakuwa kati ya Januari 14 au 15 (mwezi huu), na tutakaporudi nyumbani (Dar es Salaam) hatutakuwa na mchezo mwingine, ila mkipata nafasi ya kuona video ya mechi yetu ya kwanza, mtaamini lengo la viongozi kutuleta huku (Uturuki) limekuwa na mafanikio," Mkwasa aliongeza.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake