Imam Taifa Abdullah kutoka Boltimore, MD akitoa hotuba mbele ya waislam waliojitokeza kwenye sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa mtume muhammed S.A.W. Sherehe hizo zilifunguliwa na kijana mdogo toka Africa Mashariki Hafidh Muhammad Yousuff. Ikifuatiwa na mada mbalimbali zilizotolewa na mashehe, Al-Aman Abdul Latifa toka NYC, Imam Wassam Abdul-Baki toka Springfield, Ma. Imam Dr. Kamal Ali kutoka Westfield State. na Dr. Irshad Altheimer toka Rochester, NY. Maudhui ya hafla hii ni jinsi gani Mtume Mohammed S.A.W aliishi, alikuwa na tabia gani. Jinsi gani aliwashirikisha akina mama na vijana katika kujenga uislama. Prophet vision for the umma. Na mwisho ni mafundisho tunayotakiwa kuyafuata katika maisha yetu ya kila siku kwa ajili ya kumcha mungu. Baada ya sherehe kulikuwa na chakula kilichokuwa kimeandaliwa na familia ya Watanzania wanaoishi mji wa Springfield, MA Na New York City. Chakula kilikuwa chakutosha na kila mtu alifurahi na kusifia kuwa kuwa chakula kilikuwa kitamu.
Hafidh Muammad Yousuff akifungua sherehe hizo, Hafidh ni kijana mdogo na amejijengea heshima katika Community ya kiislam ya Springfield, MA. kwa kuwa na uwezo wa kuisoma Quran.
Watu waliojitokeza katika ukumbi wa Msikiti wa Islamc Cente Springfield, MA wakimsikiliza Imam Taifa kutoka Boltimore ,MD.
Mwenyekiti wa ccm tawi la New York Ustadh Masoud Maftah akiwa na Imam Wissam Abdul Baki wakipata ukodak kwenye sherehe hizo. Maftah na bwana Wissam wamekutana hapa baada ya kupotezana kwa miaka 32. Kwani wote walisoma Madina University huko Saudi Arabia Mwaka 1982. Na hapa ilikuwa kama surprise kukutana tena wakiwa watu wazima.
| Ny Ebra kutoka NYC akipata ukodak pamoja na mkuu wa wilaya ya Springfield na Ustadh Maftah katika HAFLA hizo Sira ya kumbukumbu za kumsifu Mtume Muhammaed S.A.W. |

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake