Tokea zama za kale binadamu wamekuwa wakitafuta asali inayozalishwa na
nyuki. Kwa azma hiyo shughuli yoyote ya ufugaji nyuki ni kuendeleza
zaidi ufanisi wa haya.
Binadamu
na nyuki hutegemeana. Kwani kwa upande wa nyuki badala ya kuwindwa na
kuuawa kwa ajili ya asali yao hutunzwa na kulindwa. Matokeo ya haya siyo
tu kupatikana kwa asali na nta bali pia kutambuliwa kwa nyuki kama
rasilimali muhimu ya kuhifadhiwa kulindwa na kustawishwa.
Ukusanyaji
wa asali na nta ni shughuli ya kijadi katika karibu bara lote la
Afrika. Wafugaji nyuki wa jadi hutumia mizinga rahisi ambayo njia ya
uvunaji asali huluta maangamizo ya makundi ya nyuki.
Kwa
hiyo iko haja ya kubadilisha njia hii kali ya ufugaji nyuki na
kuanzisha ufugaji nyuki mzuri wenye ufanisi zaidi. Huu ni ufugaji wa
kutumia mizinga ya masanduku yenye viunzi vya juu au masanduku yenye
fremu.
Shughuli yenyewe inaweza ikawa ni mradi wa kiwango kidogo ambao unaweza
kuendeshwa kirahisi. Nyuki wanasaidia kuchavusha mimea ya asili na ile
ya kilimo na biashara. Mizinga haichukui eneo lolote la ardhi na
haitegemei pembejeo kutoka nchi za nje. Yeyote anaweza akaanza ufugaji
nyuki na familia nzima ikaweza kushirikishwa. Njia nzuri ya kujifunza
juu ya ufugaji nyuki ni kufanya kwa vitendo.
Imeandaliwa na Mtandao wa Fano 2010 Products
No comments:
Post a Comment