ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 2, 2014

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, JOHN CASMIR MINJA AHUDHURIA SHEREHE ZA KUKABIDHI MADARAKA YA UONGOZI KWA KAMISHNA JENERALI MPYA WA MAGEREZA NCHINI NAMIBIA

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia anayemaliza muda wake, Evaristus Shikongo(katikati) akipokea Salaamu ya heshima toka kwa Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa na Askari wa Magereza wa Namibia(hawapo pichani) wakati wa sherehe za kukabidhi rasmi Uongozi(kulia) ni Waziri wa Ulinzi na Usalama Nchini Namibia, Mhe. Immanuel Ngatjizeko na kushoto kwake ni Kamishna Jenerali Mpya wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela. Sherehe hizo zimefanyika Februari 01, 2014 katika Chuo cha Maafisa Magereza Mahoto kilichopo nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia(hivi sasa Mstaafu) wa kwanza kulia mstari wa pili akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa Magereza wa Nchini Namibia katika sherehe za kukabidhi Madaraka ya Uongozi wa Jeshi la Magereza Nchini Namibia kufuatia kustaafu kwake kwa mujibu wa Sheria. Sherehe hizo zimefanyika Februari 01, 2014 katika Chuo cha Maafisa Magereza Mahoto kilichopo nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia
 Baadhi ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa wamesimama kabla ya Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo kupita akiwa kwenye gari Maalum la Wazi wakati akiwapungia mikono Maafisa, Askari pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Namibia ikiwa ishara  ya kuwaaga rasmi kufuatia kustaafu kwake Utumishi wa Umma akiwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia tangu mwaka1995. Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa pili kulia) ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Namibia, Luteni Jenerali John Mutwa(wa tatu kulia) ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Namibia, Inspekta Jenerali wa Polisi Denga Ndaitunga(wa tatu kulia) ni Mkuu wa Majeshi Mstaafu Nchini Namibia, Lueni Jenerali Mstaafu Martin Chalinde( wa pili kulia).
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo akiwa kwenye gari Maalum la Wazi huku akiwapungia mikono baadhi ya Maafisa na Askari wa Magereza Nchini Namibia katika sherehe za kukabidhi Madaraka ya Uongozi wa Magereza Nchini Namibia Februari 01, 2014 ambapo sherehe hizo zimefanyikia katika Chuo cha Maafisa Magereza wa Namibia kilichopo nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia.
 Gadi iliyounda Gwaride Maalum ya Wanawake, Maafisa wa Jeshi la Magereza Nchini Namibia wakipita mbele ya Mgeni rasmi huku wakiwa katika Mwendo wa haraka kama wanavyoonekana wakiwa kikakamavu Februari 01, 2014 katika Sherehe za Makabidhiano ya Uongozi wa Jeshi la Magereza kufuatia kustaafu rasmi Utumishi wa Umma kwa Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo( hayupo pichani).
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(kushoto) akimpongeza Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza Nchini Namibia, Evaristus Shikongo(kulia) mara baada ya kukabidhi rasmi Madaraka ya Uongozi wa Jeshi la Magereza Nchini Namibia Februari 01, 2014 katika Sherehe zilizofana sana nje kidogo ya Mji Mkuu wa Windhoek, Namibia( Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments: