ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 3, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA KUZALIWA CCM WILAYA YA TEMEKE

 Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kadi mmoja kati ya wanachama wapya 159, waliojiunga na CCM, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni. Wanachama hao wamejiunga na CCM katika kipindi cha maandalizi wa sherhe hizo na kufikisha idadi ya wanachama wapya 1259 waliojiunga katika kipindi hicho.
Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza matembezi ya mshikamano wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya kuku Moshi Mlaponi, aliyeibuka kidedea katika shindao la kufukuza kuku wakati wa Bonanza la michezo ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi jana jioni
Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza matembezi ya mshikamano wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni.
kwa hanari zaidi na paicha bofya soma zaidi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa wachezaji wa timu ya Makatibu Wenezi wa CCM Wilaya ya Temeke, walioshinda katika mchezo wa Soka dhidi yao na Wenyeviti wa CCM Wilaya ya Temeke katka Bonanza la michezo ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi jana jioni. Timu hiyo ilishinda bao 1-0.
 Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza matembezi ya mshikamano wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni.
 Wachezaji wa timu ya Makatibu Wenezi wa CCM Wilaya ya Temeke, wakishangilia ushindi wao huku wakiwa wamebeba Mbuzi wao juu baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni.
 Baadhi ya Wanachama wa CCM, wakicheza muziki kwa furaha wakati wa sherehe hizo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishangilia na kumpongeza James Silas, baada ya kujiunga na CCM akitokea CHADEMA, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza msanii wa mashahiri, Abdallah Nyang’anyi, baada ya kughani mashahiri yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Abdallah Nguru, akijitambulisha baada ya kujiunga na CCM akitokea CUF, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida
 Meza Kuu, ikitafakari
Baadhi ya wanachama wa CCM wakijipongeza kwa Shampeni baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.
 Meza kuu ikishiriki kula kiapo na wanachama wapya waliokabidhiwa kadi zao katika sherehe hizo jana.
 Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza matembezi ya mshikamano wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa CCM, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kibada Stendi Jimbo la Kigamboni Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, jana jioni.
 Meza kuu ikishiriki kula kiapo na wanachama wapya waliokabidhiwa kadi zao katika sherehe hizo jana.
Meza kuu ikishiriki kula kiapo na wanachama wapya waliokabidhiwa kadi zao katika sherehe hizo jana. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS AWAASA WANA-CCM DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameongoza wana-CCM wa mkoa wa Dar es salaam katika sherehe za kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika jana kote nchini.

Katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Kituo cha Mabasi Kibada maeneo ya Kigamboni Dkt. Bilal aliwataka wana-CCM nchini kuendelea kujenga imani na chama chao kwa kuwa kimeongoza kwa miaka 37 kwa amani na utulivu na kuleta maendeleo makubwa kwa wananchi.

Makamu wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM alisema pamoja na changamoto zinazojitokeza Chama hicho kimeendelea kudumisha amani na kuimarisha demokrasia nchini.

“Tunakerana…lakini hatukamatani mashati, hatupigani mapanga. Wako wachache wanaandamana lakini CCM kimetulia na kuendelea kudumisha amani na utulivu,” alisema Dkt. Bilal.

Akizungumzia kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Makamu wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa muungano wa serikali mbili unapaswa kuendelezwa kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili za muungano.

Akijibu malalamiko ya wananchi wa Kigamboni kuhusu kuchelewa kutolewa kwa fidia ya nyumba zao kufuatia mpango wa serikali wa kujenga mji wa kisasa wa Kigamboni Dkt. Bilal alisema atamwagiza Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi akutane na wananchi hao na kuwajulisha hatua iliyofikia katika kuwalipa fidia zao.

Makamu wa Rais ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Dar es salaam, alisema mpango wa kujenga mji wa kisasa wa Kigamboni ni mradi mkubwa ambao utatekelezwa na serikali na kusisitiza ni muhimu wananchi washirikishwe hatua kwa hatua katika suala zima la kuwapatia fidia zao.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
3/2/2014A

No comments: