ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 3, 2014

NAIBU WAZIRI WA FEDHA MH:MWIGULU NCHEMBA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA TUNDUMA MJINI

Naibu waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo kwa Wafanyabiashara wa Mji wa Tunduma hii leo alipokutana nao kwenye Mkutano wa ndani kwenye Ukumbi wa High Class One akizungumza nao kuhusu Maendeleo ya Biashara,Ulipaji wa kodi,Changamoto za Mpakani kwenye Ulipaji kodi,matumizi ya Mashine za EFD kwenye makato ya TRA.
 Sehemu ya Mamia ya Wafanyabiashara waliohudhuria Mkutano wa Naibu Waziri wa Fedha Mh;Mwigulu Nchemba wa Kujadiliana na kuelezana namna ya Kuimarisha Ukusanyaji wa mapato nchini.

Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Lameck Nchemba hii leo ameendelea na Ziara yake ya kikazi ya Kukutana na Wafanyabiashara ndnai ya Mkoa wa Mbeya baada ya Kufanya hivyo kwenye Mkoa wa Njombe na Ruvuma wiki iliyopita.
Hii leo Mh:Mwigulu  amezungumza na mamia ya wafanyabiashara wa Mji wa Tunduma kuhusu nafasi yao ya Kukuza Ukusanyaji wa mapato kwa kaucha kukwepa kulipa kodi,Kuacha kupitisha bidhaa kimagendo kwenye mpaka wa Nchi ya Tanzania na Zambia.Wafanyabiashara Wakitanzania wasio wazalendo wa Kulipa kodi wamekuwa wakitumia mwanya wa Mpaka kuvuka kufanya biashara Zambia na makazi yao yapo Tanzania kitu kinachopelekea ukusanyaji wa Mapato kuwa Mgumu kwa TRA na taasisi husika. Serikali imeamua kufanya maridhiano na Serikali ya Zambia kuhakikisha kunakuwepo na Mpaka uliotenganishwa kwa Mita 50 kila upande wa Nchi hizi mbili ilikudhibiti ukwepaji wa kulipa kodi na biashara ya Magendo.
Naibu waziri pia alitumia nafasi kuwaelimisha Wafanyabiashara umuhimu wa kutumia mashine za EFD kwenye kurahizisha ukusanyaji wa mapato na kukuza biashara zao.Mbali na hayo wafanyabiashara walipata nafasi ya kutoa mawazo,maoni yao kwa Naibu waziri wa Fedha namna ya Kuimarisha Ukusanyaji wa mapato,Uelewa wao kuhusu Mashine za EFD na Ushirikiano watakao onesha kwenye Kudhibiti ukusanyaji mapato mpakani Mwatanzania na Zambia.
Picha na Habari Kwanza Blog

No comments: