ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 19, 2014

SERIKALI YAWATANGAZIA NEEMA WAALIMU

WALIMU WAAHIDIWA KULIPWA MADENI YA MAPUNJO YA MISHARAHA YAO.
SERKALI imewaahidi walimu kote Nchini kuwa itawalipa Madai yao yote mwaka huu zikiwa ni juhudi za kuinua na kuongea ari ya utendaji wa walimu hao na kuyafikia malengo iliyojiwekea ya matokeo makubwa sasa (BRN).

Kauli hiyo ilitolewa kwa nyakati tofauti na Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwl. Jenista Mhagama wakati akiongea na walimu katika shule za Msingi Tuwemasho, Matemanga Sekondari na Kiuma Bonite Sekondari Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na kuongeza kuwa tayali Wizara yake imeomba Shilingi Bilioni 61 ili zitumike kulipia madeni hayo.
Akifafanua taarifa hiyo Mwl. Mhagama alisema kuwa halai hiyo imetokana na Serikali kusikia kilio cha muda mrefu amvacho kimekuwa kikitolewa na Walimu hapa nchini hali amabayo iliisukuma kutuma wataalamu wake kufanya uchunguzi wa kero hizo nakubaini uhalisia wa madai hayo.
Alisema kufutia hali hiyo kuanzi sasa walimu wanapaswa kuwajibika katika ufundishaji na kuahakikisha wanamaliza Mitaala na vipindi walivyo pangiwa ili kuongeza ufaulu kwa watoto waliopewa mamalaka ya kuwalea.

No comments: