ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 18, 2014

TANZANIA: URAIA PACHA NA DIASPORA KUPATA HAKI YA KUPIGA KURA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA: BUNGE LA KATIBA: URAIA PACHA NA DIASPORA KUPATA HAKI YA KUPIGA KURA
Kuna waTanzania zaidi ya millioni mbili (2,000,000) wanaoishi nje ya Tanzania. Watanzania hawa ni nguvu kazi, wazalendo na wanamapenzi ya moyoni kwa nchi yao.  Wengi wa watanzania hawa walizaliwa Tanzania, wamesomea Tanzania, wana familia Tanzania na mioyo yao ni Tanzania.
Watanzania hawa wanasoneneka kupoteza uraia wa KUZALIWA kwa sababu tu wamebahatika kupata uraia wa nchi nyingine ili kuweza kurahisisha jinsi ya kupata elimu, huduma za afya na kufanya kazi kwenye mataifa hayo wanayo ishi.
Pia, katika waTanzania hawa kuna nguvu kazi madaktari, wanasheria, mainginia, wenye vipaji vya michezo, wenye miradi na wajuzi wa fani mbali mbali ambao ni hazini kubwa kwa taifa letu. Hawa waTanzania wanashindwa kuwekeza nyumbani kwa kuwa wanakosa haki ya kuitwa waTanzania huku UHALISIA wamezaliwa Tanzania.
Saini zote zinazo wekwa humu zinaomba Bunge la Katiba na wajumbe wote wa Bunge hili tukufu kupitisha uraia pacha na wajasilimari hawa million mbili (2,000,000) wapate haki ya kupiga kura na kuchangia ujenzi wa taifa letu.

Ni imani ya kila mTanzania na wana diaspora kuwa busara na hekima vitatumika katika hili na siasa kuwekwa kando.
ITIKADI PEMBENI TUTENGENEZE KATIBA KWA MANUFAA YA WATANZANIA
TANZANIA TANZANIA, NAKUPENDA KWA MOYO WOTE...

No comments: