ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 19, 2014

UKRAINE YAWAKA MOTO


Upinzani huko Ukrain umeapa kutotoka uwanja wa uhuru wanakoendeleza maandamano hayo.
Wakuu kutoka umoja wa Ulaya wameshtumu vikali rais wa Ukrain Viktor Yanukovych, kwa makabiliano makali baina ya polisi na waandamanaji yanayoingia siku ya pili sasa .

Waziiri Mkuu wa Poland , Donald Tusk, amesema atapendekeza Ukrain iwekewe vikwazo vya kiuchumi huku yule wa Sweden Carl Bildt akiongeza kuwa damu ya watu 25 waliokufa katika maandamano hayo iko mikononi mwa Yanukovych.
Vile vile wameutaka upinzani kuzuia machafuko zaidi ambayo yanasambaa kwengineko nchini humo

No comments: