Bidhaa Mbalimbali za Kilimo Zinazozalishwa na Vijana wa Mkoani Dodoma Ambao watazionyesha kwa Wakazi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya Jirani.Bw Jackson Audiface Akielezea Zaidi Kuhusu Maonyesho hayo Yatakayofanyika Mkoani Dodoma.Hapa Akiwa Ameshika Mafuta yanayozalishwa na Vijana wajasirimali wa Mkoani Dodoma jana Wakati wajasiriamali hao walipotembelea Ofisi za Kampuni ya Aj It Development Kwajili ya Kujisajili ili kushiriki Katika Maonyesho ya Kazi za Vijana wajasiriamali Yatakayofanyika Mkoani Dodoma
Kampuni ya AJ IT DEVELOPMENT inatarajia kufanya Maonyesho ya Tatu ya Kazi za vijana Wajasiriamali Yanayofahamika kama Tanzania Youth Enterprenuership Program (TAYEP) Yanayotarajiwa Kufanyika April 3 - 5 April, 2014 Mkoani Dodoma.
Kwa
mujibu Mkurugenzi wa Kampuni ya AAj It Development Bw Jackson
Audiface, Maonyesho hayo ya aina yake kufanyika nchini Tanzania yenye
lengo la Kuzitangaza Kazi za Vijana Wajasiriamali .
“Maonyesho
haya Yalianzishwa Kwa Lengo la Kutatua changamoto zote zinazowakabili
Vijana wajasiriamali Pindi wanapojishugulisha Katika Shuguli zao za
Ujasiriamalia.
Aliongeza
kuwa washiriki watapata Ya Kuzitangaza Kazi zao,Kujua Taratibu
Mbalimbali na Namna Ya Kuingiza bidhaa zao Kwenye Masoko Mbalimbali kwa
Wingi zaidi.Namna ya Kupata vibali Mbalimbali vya Kufanyia Biashara
Kutoka Mamlaka Mbalimbali za serikali.Kupata elimu namna ya Kuziboresha
Bidhaa zao ziendane na soko pia Kukidhi viwango na Matakwa ya
Wateja.Kuwakutanisha na wadau Mbalimabali wa Vijana na Kujua taratibu
namna ya Kushirikiana na Wadau hao katika Kuboresha Bidhaa zao.
Akizungumza
mfumo utakaotumika kuendesha Maonyesho hayo Bw Jackson Audiface Alisema
Kila Mshiriki Atapata Fursa ya Kuonyesha Kazi yake na Kuilezea Kwa Kina
pia na Changamoto Anazokabiliana nazo kazi kazi zao za Ujasiriamali.
Walengwa wakuu wa Maonyesho hayo ni Vijana Kutoka Mkoani Dododma Hususani Vijana Kutoka Vyuo Vilivyoko Mkoani Dodoma.
Washiriki
wa Maonyesho hayo wanatarajiwa kuwa 3,000 Ambapo Vijana 250 Wataonyesha
Kazi zao Zikiwemo Bidhaa za Kilimo ,Teknolojia ya Habari,Sayansi ya
Kompyuta,Utalii wa Ndani na Ufugaji.
“Tunaomba makampuni na mashirika Ambao ni Wadau wakubwa wa Maendeleo ya vijana kutumia fursa
hii Kufadhili Maonyesho Hayo ili waweze Kujione Fursa Mbalimbali
Wanazofanya Vijana. Pili kujitangaza, na kutangaza bidhaa na huduma
zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao
Mgeni rasmi wa Maonyesho Hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Mizengo Pinda
No comments:
Post a Comment