Naibu
Waziri wa wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi Kaika Saning’o Telele
akifungua warsha ya kimataifa kuhusu maendeleo, miundo mbinu na vituo
vya maji. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wizara ya maji Eng. Bashir
Mrindoko, anayefuatia aliyevaa miwani Katibu Mkuu msaidizi maendeleo ya
maji na umwagiliaji nchini Malawi Mrs Erica Maganga, anayefuatia
Mhandisi Mkuu wizara ya maji Zimbabwe Ms. Tatenda Mawokomatanda, kushoto
kwa Naibu waziri Afisa Taaluma kutoka UN yenye ofisi zake nchini
Ujerumani Dkt. Mathew Kurian. Warsha hiyo ya kimataifa inawakutanisha
wanataaluma mbalimbali inayofanyika Siku mbili katika hoteli ya Ledger
Plaza Bahari Beach, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wizara ya maji Eng. Bashir Mrindoko akifafanua jambo wakati wa
mapumziko katika warsha ya kimataifa kuhusu maendeleo, miundo mbinu na
vituo vya maji kulia
anayesikiliza ni Naibu Waziri wa wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi
Kaika Saning’o Telele, anayefuatia kwa Naibu waziri ni Mhandisi Mkuu
wizara ya maji Zimbabwe Ms. Tatenda Mawokomatanda, na Kushoto kwa
Mrindoko ni Katibu Mkuu msaidizi maendeleo ya maji na umwagiliaji nchini
Malawi Mrs Erica Maganga.
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha ya kimataifa iliyofanyika katika hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach, Nchini Tanzania. Picha na Chris Mfinanga.
No comments:
Post a Comment