Kamishna
Msaidizi wa Madini ,Wizara ya Nishati na Madini , Mhandisi Hamis Komba
akiongea jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Thailand Mhe.
Srirat Rastapana mara baada ya kufungua maonesho ya 53 ya “Bangkok Gems
& Jewelry Fair” mapema leo. Nyuma ya Kamishna ni Bw. Edward Rweymamu
ni Mthamini wa Madini ya Almas Wizara ya Nishati na Madini. Kushoto
Mhe. Dora Mushi mfanyabiashara wa madini kutoka Arusha.
Rais
wa Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand Bw. Somchai
Phornchindarak akiangalia madini ya Almas katika banda la Tanzania.
Anamwelekeza jambo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vito ya Shirikisho la
Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Bw. Gregory Kibusi. Wengine wanaoshuhudia
ni baadhi ya ujumbe wa Tanzania unaoshiriki maonesho hayo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sam Mollel wa
pili kulia akionesha Hati ya Maridhiano ya kuendeleza ushirikiano wa
tasnia ya madini ya vito na usonara baada ya kusaini kati yake na Rais
wa Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand Bw.
Somchai Phornchindarak. Wanaoshuhudia ni Kamishna msaidizi wa Madini,
Mhandisi Hamis Komba (Wa kwanza kulia) na Makamu wa Rais wa Shirikisho
la madini na usonara la Thailand Bw. Peter Brooke.
Ujumbe
wa Tanzania katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya Bangkok katika picha
ya pamoja na Rais Rais wa Rais wa Shirikisho la madini ya vito na
usonara la Thailand Bw. Somchai Phornchindarak (aliyeshika kinyago cha
mamba kilichochongwa kutokana na mawe ya madini yanayopatikana nchini
Tanzania. Kinyago hicho kimechongwa na Kituo cha 'Tanzania Geomological
Center' kilichopo Arusha.) Wa tatu kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa
Shirikisho la madini na usonara la Thailand Bw. Peter Brooke.
Balozi
wa Afrika ya Kusini nchini Thailand Mhe. Ruby Marks (katikati) katika
picha ya pamoja na wafanyabiashara ya madini( wa kwanza kushoto, Bw. Sam
Mollel mwakilishi kutoka Tanzania Geomological Center (wa tatu kulia)
Bw. Musa Shanyangi Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Kamati ya Vito ya
Shirikisho la Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Bw. Gregory Kibusi.(nne
kulia).
Na Asteria Muhozya, Bangkok,
Nchi
washiriki wa Maonesho ya 53 ya Kimataifa ya “Bangkok Gems & Jewelry
Fair” wametakiwa kuyatumia maonesho hayo kujenga mitandao ya biashara ya
madini ya vito na usonara ili kusaidia kuinua uchumi na mapato ya nchi
zao.
Akizungumza
katika ufunguzi wa maonesho hayo, yaliyoanza leo jijini Bangkok, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Thailand, Mhe. Srirat Rastapana, ameeleza
kuwa, maonesho hayo ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa biashara, ukuaji
wa uchumi na uwekezaji kupitia sekta ya madini.
Vilevile
alieleza kuwa, mbali ya kujenga mtandao wa kibiashara, amewataka
washiriki kuyatumia maonesho hayo, kubadilishana uzoefu na teknolojia
zinazotumika katika sekta hiyo.
Akielezea
uzoefu wa nchi hiyo katika sekta ya madini ameongeza kuwa, madini ya
vito na usonara yamechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi
hiyo na kuongeza pato la taifa hivyo, serikali ya Thailand inayapa
kipaumbele kikubwa maonesho hayo kutokana na mchango wake katika
maendeleo ya taifa.
Akielezea
mafanikio katika sekta hiyo, ameongeza kuwa, madini na vito nchini
Thailand yamesaidia kuzalisha watalaamu zaidi ya milioni moja katika
sekta ikiwa ni pamoja na kuongeza pato la taifa ambapo kwa mwaka 2013
Serikali iliingiza kiasi cha zaidi ya dola za Marekani bilioni moja.
“
Tunataka kuona Bangkok inakuwa kituo kikubwa cha biashara ya madini, na
tunakuwa bora katika kutengeneza bidhaa zinazotokana na madini
duniani. Alisema”.
Kwa
upande wake Kamishna msaidizi wa Madini, Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Hamis Komba ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika
maonesho hayo ya 53 amesema kuwa, Serikali imeimarisha ushirikiano na
wafanyabiashara wa madini na wachimbaji ili kuiwezesha seka ya madini
kuleta tija kwa taifa ikiwemo kuvutia uwekezaji na kuweka mazingira
mazuri ya kufanya biashara ya madini ya vito na usonara.
Aidha
ameongeza kuwa, tayari Serikali imeondoa kwa muda zuio la kusafirisha
madini ghafi aina ya Tanzanite ili kuwezesha uwepo wa Tanzanite katika
maonesho ya 53 na katika banda la Tanzania, jambo ambalo linarahisisha
na litawasaidia wafanyabiashara wa Tanzanite kufanya biashara kimataifa.
Vilevile
ameongeza kuwa, tayari Serikali iko katika hatua za kukusanya maoni
kutoka kwa wadau kuhusu Sheria ya Uongezaji thamani madini jambo
ambalo litasaidia kuboresha sekta hiyo, hivyo, kukamilika kwa sheria
hiyo kutawanufaisha wadau wote wa sekta ya madini wakiwemo
wafanyabiashara, masonara wachimbaji na Serikali jambo ambalo
litachangia katika ukuaji wa uchumi na kuongeza pato la taifa kupitia
sekta ya madini kama ilivyo kwa nchi nyingine ambazo zimefanikiwa
katika sekta hiyo.
Kuhusu
suala la utoroshaji wa madini, Kamishna komba amesema kuwa, sheria
pekee haiwezi kuzuia tatizo hilo, hivyo amewataka wafanyabiashara kuwa
wazalendo na kufanya kazi kwa kushirikiana na serikali ili sekta ya
madini iweze kunufaisha pande zote na kuwanufaisha watanzania wote.
Wakati
huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania
(TAMIDA) Sam Mollel amewataka wafanyabiashara kuyatumia maonesho ya
kimataifa kuonesha bidhaa zao kwa kuwa kuna mafanikio makubwa, mbali
ya kufanya biashara kwani watajifunza mengi kuhusiana na madini, kwa
kuwa yapo mengi ya kujifunza ikiwemo kujifunza kutoka kwa waoneshaji
wengine.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Vito ya Shirikisho la Wachimbaji
Tanzania (FEMATA) Bw. Gregory Kibusi ameishukuru Serikali kuwawezesha
kushiriki maonesho hayo, kwani kufika kwao kumewafunza mengi ikiwemo
kupata uzoefu
kuhusu
sekta hiyo ikiwemo kujua tecknolojia zinazotumika kukata madini, kujua
umuhimu wa kukata madini, kujua bei, fursa ya kukutana na
wafanyabiashara wa kimataifa jambo ambalo limechangia kuwapa elimu
zaidi kuhusu madini na vito kutoka nchi zilizofanikiwa katika biashara
ya madini ikiwemo wenyeji Thailand, Marekani, India na Sirilanka lakini
pia uzoefu kutoka nchi za kiafrica kutoka Senegal, Ghana, Madagasca,
Nigeria, Cameroon na nchi nyingine za nje ya Africa.
No comments:
Post a Comment