ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 3, 2014

ZANZIBAR KUANZISHA CHUO CHA MAFUNZO YA AMALI KWA WANAWAKE KWA KUSHIRIKIANA NA CHUO CHA BAREFOOT CHA INDIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipokea zawadi mara alipowasili katika Chuo cha Mafunzo ya Amali kiitwacho Tilonia, Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan akiwa katika siku ya pili ya ziara yake nchni India pamoja na ujumbe aliofuatana nao.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim (kulia) kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitiliana saini makubaliano ya uanzishwaji wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake na Chuo cha Barefoot cha India ambapo muanzilishi wa Chuo hicho Bw. Bunker Roy alitia saini (kulia). Saini hiyo ilifanyika wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara rasmi nchini India na ujumbe wake.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Affani Othman Maalim (kulia) akibadilishana hati za makubaliano na Bw. Bunker Roy baada ya kutiliana saini makubaliano ya uanzishwaji wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Chuo cha Barefoot cha India, saini hiyo ilifanyika wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika ziara rasmi nchini India na ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Bw. Bunker Roy Muanzilishi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali kwa Wanawake katika Kijiji cha Tilonia Wilaya ya Ajmer Jimbo la Rajastan pamoja na Balozi wa India nchini Tanzania Debnath Shaw (kulia) baada ya saini ya makubaliano ya uanzishwaji wa chuo kama hicho Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Bw. Bunker Roy.
[Picha na Ramadhan Othamn, Ikulu]

2 comments:

Anonymous said...

Hizo pesa munazozitumia kwa misafara yenu zinatosha kujenga vyuo kumi kama hicho cha wahindi. Wao wenyewe njaa tupu. Itakuwaje watusaidie sisi!!!.

Anonymous said...

umenena mdau wa mwanzo sadakta lakin si unajua tena wakisafiri wanapata posho zao so na kuuuza nchi ambayo hawana uchungu nayo si tatizo kwao ndo maana tunasema tunataka mamlaka kamili ya nchi yetu tuendeshe wenyewe na hawa wakuu mafisadi waende mrima wakapewa vyeo vyao wakatik tukiwa na maamlaka yetu kamili hatuwataki wakuu kama hawa