Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Wana Habari
hawapo Pichani kuhusu muenendo wa Bunge la Katiba unaoendelea Mjini
Dodoma.
Balozi Seif akizungumza na Wana Habari waliojumuika na Baadhi ya Mawaziri wa SMZ katika Ukumbi wa TAMISEMI Mjini Dodoma.
Baadhi
ya wana Habari wakisikiliza Hotuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo Pichani akielezea mchakato mzima wa
maendeleo ya Bunge Maalum la Katiba linaloendelea Mjini Dodoma.
Wapiga
Picha wa Vyombo mbali mbali vya Habari wakiwa kazini kwenye Mkutano wa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waandishi wa
Habari katika Ukumbi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Mjini Dodoma.(Picha na Hassan Issa – OMPR)
Na. Othman Khamis. OMPR.
Wabunge
wa Bunge Maalum la Katiba wana wajibu wa kutekeleza kazi zao kwa mujibu
wa Kanuni walizojiwekea za kuendesha Bunge hilo ili kiuwa mfano mwema
wa matendo mazuri mbele ya jamii ya Watanzani kutokana na dhima
waliyokabidhiwa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati
akizungumza na wana Habari mbali mbali wanaoripoti matukio ya Bunge la
Katiba hapo katika Ukumbi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mjini Dodoma.
Balozi
Seif alisema vitendo vya uvunjifu wa amani kila siku ili Bunge Maalum
la Katiba liahirishwe kwa sababu za Kisiasa na msimamo ya kisiasa
inayofanywa na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo si jambo jema.
Alisema
mchakato huo wa Bunge Maalum la Katiba umekuwa ukishuhudiwa na
Wananachi walio wengi Nchini kutawaliwa na wanasiasa wanaoonyesha
dhahiri nia zao za kutaka kuvunja Muungano kutokana na kauli zao.
Alieleza
kwamba kaulio nyingi zinazotolewa na kushuhudiwa na Wananchi kupitia
vyombo vya Habari zimekuwa na muelekeo wwenye kuchionganisha Wananchi wa
pande mbili za Muungano.
“Inasikitisha
sana kuona baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba wanaendeleza ushabiki
wa Kisiasa ndani ya Vikao vya Bunge hilo kwa kutengeneza mbinu za
kuongeza muda wa Vikao wakisahau kwamba kodi za Wananchi zinapotea bila
ya kufanya kazi zilizokusudiwa kufanywa na Waheshimiwa sisi Wajumbe “.
Alisema Balozi Seif.
Balozi
Seif alifahamisha kwamba pamoja na hatua nzuri iliyofikiwa na Wajumbe
wa Bunge hilo ya kujadili Rasimu ya Katiba na kuweza kubadilisha,
kuboresha, kuongeza au kupunguza lakini bado zipo changamoto
zinazolikabili Bunge hilo.
Alizitaja
baadhi ya change moto hizo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa uvumilivu
miongoni mwa Wajumbne wa Bunge Maalum, Bunge kutawaliwa na hisia za
kisiasa zaidi badala ya kuweka maslahi ya Taifa mbele pamoja na kuwepo
kwa vikundi vya watu wachache wasiotaka mchakato huo wa Katiba Mpya
kuendelea kutokana na utashi wa kisiasa.
Akizungumzia
suala la Mikutano ya hadhara inayoanza kuchukuwa sura mpya ya kutaka
kugawanywa Wananchi ndani ya kipindi hichi cha mchakato wa Bunge la
Katiba Balozi Seif aliwatahadharisha Wananchi kuwa macho na tabia hizi
zinazoonekana kutaka kuleta mgawanyiko wa Jamii kati ya Tanzania Bara na
Zanzibar.
Alisema
kauli za Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa kuwataka Wananchi wa Upande
mmoja wa Muungano kuacha shughuli zao za Kimaisha na kurudi katika
makazi yao waliyozaliwa ni kuashiria jinsi viongozi hao walivyo na nia
mbaya katika kuvunja Umoja wa Nchi na Muungano uliopo hivi sasa.
Balozi
Seif alieleza matumaini yake kwamba Muungano uliopo hivi sasa wa
Tanzania itaendelea kudumu, kuwepo na kuendelea kwa kipindi kirefu
kijacho kwa vile bado unaridhiwa na kukubalika na jamii ya wananchi
walio wengi ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba na
Uongozi wake kwa kazi waliyoifanya ya kukusanya maoni ya Wananchi
pamoja na kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya
Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohd Shein kwa muongozo wao
wa muelekeo wa mchakato huo.
Alisema
dhamira ya Viongozi hao iko wazi na dhati katika kuhakikisha Taifa hili
la Tanzania linapata katiba Bora ya Wananchi kupitia Bunge Maalum la
Katiba lililoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya
83, toleo la Mwaka 2012.
“Kazi
iliyopo mbele yetu ni Bunge Maalum kukaa kama Kamati ambazo ni 12 ili
kujadili kwa kina rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili kupata
Rasimu nzuri itakayoleta faida kwa Wananchi “. Alifafanua Balozi Seif.
Balozi
Seif Ali Iddi aliwashukuru watendaji wa vyombo mbali mbali vya Habari
kwa kazi nzito wanayoendelea kuifanya katika kuwapatia Taaluma na
Habari Wananchi juu ya masuala tofauti ikiwemo mchakato wa Katiba
unaoendelea Mjini Dodoma.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaasa Wanahabari hao kwamba ni vyema
wakaelewa kuwa bado wanakabiliwa na dhima ya kuielimisha Jamii umuhimu
wa kuichunga amani iliyopo hapa Nchini.
“Napenda
muelewe kwamba bado mna dhima ya kuielimisha jamii umuhimu wa kuichunga
amani iliyopo Nchini “. Alisisitiza Balozi Seif.
Akijibu
baadhi ya maswali ya wana Habari hao likiwemo lile linalodaiwa kwamba
Zanzibar imevunja Katiba kwa kubadilisha baadhi ya vifungu vya sheria na
ikiwemo Zanzibar kuitwa Nchi, Balozi Seif aliwatoa hofu wana habari hao
kwamba Zanzibar kamwe haijavunja katiba kwa vile haina Utaifa.
Alisema
Utaifa uliopo na unaoendelea kutumiwa na kujuilikana ni ule wa
Utanzania akatolea mfano masuala ya Kimataifa yanashughulikiwa na
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Hebu
nikuulizeni Nyinyi Waandishi mna kumbu kumbu yoyote mnayoijua au
kuikumbuka kwamba kuna Balozi yeyote wa Zanzibar katika Mataifa ya
Kigeni ? “. Aliuliza Balozi Seif.
1 comment:
Mimi sielewi viongozi wa Chama changu wakisema Bunge lisitawaliwe na jazba na itikadi za kivyama huwa wanakusudia nini? Imesemwa hivi si mara moja wala mbili kuwa Chama chetu msimamo wake ni Siri kali mbili (2) na kauli hii imekuwa inajengewa hoja na kukingiwa kifua kila siku ndani na nje ya Bunge hili, hata Mwenyekiti wetu amesema wazi kuwa Siri kali tatu (3) zisije hadi hapo yeye atakapostaafu, kwa sasa twende na hizi hizi mbili (kwa mujibu ya itikadi yetu). Hapa sasa Mh Seif Iddi unachokataza ni itikadi za vyama zisiingizwe Bungeni au itikadi ya vyama vyengine mbali ile ya Chama chetu. Maana naona hiyo itikadi yetu ndio imekuwa inalazimishwa kwa lazima hata kama wananchi hawataki (kwa mujibu wa jaji Sinde) WANASIASA TWAMBIENI MANATAKA NINI?? MSITUVUNGE
Post a Comment