Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Halima Mdee, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo
la Kawe (CHADEMA), akiwa haamini kinachoendelea kwenye ukumbi wa bunge
wakati wajumbe wa bunge hilo walipocharuka jana na hivyo kumlazimisha
mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Pandu Ameir Kificho, kuliahirisha kwa
muda ili kuepusha uchafuzi zaidi wa "Hali ya Hewa"
Hebu muone uyu naye.
Mbunge Moses Machali
Christophe Ole Sendeka, naye hakuwa nyuma kwenye "sheshelumbe" la Jana Alhamisi Machi 6, 2014
Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda(Katikati) na viongozi wengine, wakimsikiliza Katibu
wa Bunge, Thomas Kashilila baada ya kutokea kizaa zaa
Wajumbe wa bunge maalum la Katiba, wakitoka ukumbini baada ya kuahirishwa kwa muda kufuatia sintofahamu iliyotokea
BUNGE maalum la Katiba, Jana Alhamisi Machi 6, 2014,
liligeuka uwanja wa “Mapambano” kama ile vita iliyotikisa
ulimwengu, vita ya Kosovo kule eneo la Balkan.
Hata hivyo sio mapambano ya ngumi bali Majibishano makali
yalizuka wakati wajumbe wakiendelea kujadili kanuni zitakazokuwa dira ya
kuliongoza bunge hilo maalum, ambalo linaketi
pale “mjengoni” kwenye ukumbi wa Bunge la Tanzania
mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo,
Pandu Ameir Kificho, alilazimika kuliahirisha bunge hilo kwa takriban masaa manne, baada ya
sintofahamu iliyohanikiza ukumbi huo unaochukua takriban watu 700.
Malumbano hayo yalikuwa ni kati ya wajumbe na mwenyekiti
wakati mwingine wajumbe kwa wajumbe, picha kadhaa zilizopigwa na waandishi wa
habari wakati sakata hilo likiendelea, zinaonyesha, wajumbe kama vile,
Christopher Ole Sendeka, Waziri wa sheria na katiba wa Zanzibar, Abubakar
Khamisi Bakari,Moses Machali na wajumbe wengine kadhaa, wakitoa maneno makali
dhidi yao wao wenyewe na wakati mwingine wakimtuhumu mzee Kificho kwa
upendeleo.
Baadhi ya wajumbe wa bunge hilo,
kama Halima Mdee, kuna wakati alionekana akiwa
ameshikwa na butwaa asiamini kinachoendelea ukumbini.
Kasheshe hizo zinajiri huku wajumbe hao wakiwa hata
kuapishwa bado, na wachambuzi wa mambo wanabashiri kuwa hata mpango wa Ikulu wa
kutaka hotuba ya uzinduzi wa bunge hilo
kufanyika wiki hii huenda usifanikiwe kwani hata uchaguzi wa mwenyekiti bado
kufanyika na kazi ya kuapisha wajumbe hao zaidi ya 600 huenda ikachukua hadi
siku tatu.
No comments:
Post a Comment