Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David A. Misime - SACP
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi
la Polisi Mkoani Dodoma linashikilia arobaini na tano kwa makosa
mbalimbali ya uhalifu katika msako wa wahalifu uliofanyika tarehe kati
ya tarehe 27/02/2014 hadi 01/03/2014.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David
A. Misime - SACP amesema tarehe 27/02/2014 walikamatwa jumla a
watuhumiwa 42 kwa makosa mbalimbali ikiwemo pombe ya moshi lita 11 na
nusu, mitambo ya gongo miwili, machicha ya kutengenezea gongo lita 50 na
bangi misokoto 50 kufuatia msako uliofanywa na mtandao wa Polisi
wanawake TPF-Net.
Kamanda
Misime aliongeza kuwa katika tarehe 01/03/2014 alikamatwa Shafii s/o
Husein, miaka 25, kabila Mrangi, muuza matunda na mkazi wa Chang’ombe
Manispaa ya Dodoma akiwa na jumla ya Noti bandia 24, kati ya hizo noti
23 zote zinafanana zenye namba BU 7273435 na noti moja ina namba BE
9463738 za elifu kumi zinazoonyesha kuwa na thamani ya 240,000/=
akijaribu kuziingiza katika mzunguko wa fedha kwa njia ya M- Pesa.
Pia
Kamanda misime alisema kuwa alikamatwa Haroun s/o Dotto, miaka 22,
kabila Mgogo, Mkulima na mkazi wa kijiji cha Matumbulu Manispaa ya
Dodoma akiwa amepanda bhangi kiasi cha robo heka katika shamba la
mahindi, Wilaya ya Chemba amekamatwa mtu mmoja akiwa amelima Bangi kiasi
cha nusu hekari lililoharibiwa baada ya kukamatwa.
Aidha
Kamanda Misime alisema msako bado unaendelea katika Wilaya zote Mkoa wa
Dodoma. pia amewashukuru wananchi kwa jinsi wananyoendelea kutoa
ushirikiano na jeshi hili lililofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.
No comments:
Post a Comment