ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 3, 2014

KIJANA ALIYEGEUKA ALBINO BAADA YA KUATHIRIKA NA MATUMIZI YA DAWA AINA YA METAKELFIN.

Bw.Hafidh Masokola Damson ambaye alibadilika na kuwa Albino kutokana na matumizi ya dawa za Malaria baada ya kuzitumia mnamo mwaka 2010,Kwa maelezo yake mara baada ya kunywa dawa aina ya Metakelfin alianza kubabuka ngozi ya mwili wake huku magamba yakitoka mithiri ya nyoka katika mwili wake.

Hafidh Masokola kabla ya kubadilika kuwa mlemavu wa ngozi Albino.
Kwa uthibitisho wa habari hii waweza kumpigia kwa simu ya kiganjani 0767 298 348 au 0658 298 348.

3 comments:

Anonymous said...

Tatizo liko katika uthibiti duni wa dawa hizi.Kumekuwa na counterfeit medication nyingi sana nchini,ni Mungu tu ndio anaesaidia kuwalinda wa Tanzania.
Wafanyabiashara wameshakuwa wauwaji wamefikia hatua ya kutengeneza dawa feki kwa matumizi ya binadamu.

Anonymous said...

Inasikitisha sana jamani, sasa haijulikani hizo dawa alipewa hospitali au alinunua mtaani.Nafikiri kabla mtu hajatumia dawa lazima aangaliwe kama ana alergy sijui kama hili huwa linazingatiwa.Kuna Dada alipata reaction ya dawa za malaria sikumbuki ilikuwa aina gani ngozi yake ilipata mabaka kama chui na aliambiwa itachukua muda kupona ila kweli baada ya muda wa zaidi ya miaka mitano taratibu ngozi ilianza kurudia rangi yake.Ingawa psychologicaly aliathirika sana.Hili ni swala linaweza kudhibitiwa na wizara husika na wananchi waelimishwe hatari ya kunywa dawa za mitaani.

Anonymous said...

Dawa kama za malaria zingeanza kutolewa bure tu maana kuna wananchi ambao hana hata pesa ya ununua chakula sasa atakwenda kweli kununua dawa ya malaria jamani? Na hata akipata hiyo dawa, lazima atanunua zile ambazo ni rahisi kulingana na uwezo wake masikini. Pole sana kaka.