Korea Kaskazini inatuhumiwa kurusha makombora mawili ya masafa mafupi
siku ya Jumatatu ya leo katika eneo la bahari katika pwani ya mashariki
ya Korea.
Habari kutoka shirika la Reuters zikiikariri wizara ya ulinzi ya Korea Kusini zimesema hili ni tukio la pili baada ya lile lililofanyika wiki iliyopita.
Shirika moja la habari la Korea Kusini linasema makombora hayo ni aina ya Scud-C yanayoweza kwenda umbali wa kilomita 500 baada ya kufyatuliwa. Umbali huo inamaanisha una uwezo wa kuyafikia maeneo yatakayolengwa nchini Korea Kusini ama Japan.
Makombora hayo yamefyatuliwa katika kipindi ambacho Marekani na Korea Kusini zinafanya mazoezi ya pamoja ya kila mwaka, suala ambalo Korea Kaskazini inahofia kuwa ni mazoezi ya vita

No comments:
Post a Comment