Hatimaye
Mama aliyetoroka na mtoto aliyeungua moto apatikana kupiga simu katika
Chombo cha Mbeya yetu Blog kuwa yupo Njombe kwa baba mzazi wa mtoto huyo
nakuomba radhi kuwa aliondoka bila kuaga kesho saa nane mchana atakuwa amerudi
na mtoto huyo
Mama huyo
amejitokeza baada ya mtandao wa Mbeya yetu kuandika mapema leo kwamba alikuwa
ametoweka bila Taarifa zozote, Akiongea na Mbeya yetu amedai kwamba yeye
aliondoka ili akashauriane na wazazi wa Mtoto huyo ili waone ni jinsi gani
watamsaidia lakini alipo hojiwa amejikanyaga kanyaga na kuongea bila kuwa na
uhakika na kile anacho zungumza.
Hata hivyo
hapo kesho atafanyiwa mahojiano ya kina na kuona ukweli ukowapi kwa kuwa anatia
mashaka na maelezo yake, Tunaendelea kusisitiza kuwa Kama kuna Mtu anahitaji
kumchangia mtoto huyo asifanye hivyo kwa kuwa mama huyo kasha onesha wasiwasi
na kuondoa imani watu.
Habari zaidi zitakuja
Huyu ndiye Mama Mkubwa wa Mtoto Adolotea Nyavike bi. Salome Kiegu(35) ambaye alitoweka na mtoto huyo kusiko julikana huku wasamalia wema wakitaka kutoa misaada.
No comments:
Post a Comment