ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 9, 2014

Rais Kikwete awaongoza viongozi mbali mbali na mamia ya waombolezaji kumfariji Mh. Sophia Simba


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba kufuatia kifo cha mwanaye Marehemu Leeford Simba huko Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Familia ya Marehemu Leeford Simba wakiwa ni wenye huzuni mkubwa kwa kuondokewa na mpendwa wao.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pole na kumfariji Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba kufuatia kifo cha Mwanaye Leeford Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leedford anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa ndugu wengine wa Marehemu Leeford Simba.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Neema Mathew(kulia) na waombolezaji wengine kufuatia kifo cha Mumewe Leeford Simba kilichotokea juzi. Marehemu Leeford Simba ni mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe. Sophia Simba kufuatia kifo cha mwanaye,Marehemu Leeford Simba,Masaki jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimpa mkono wa pole na kumfariji Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba kufuatia kifo cha Mwanaye Leeford Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leedford anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisaliana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge),Mh. William Lukuvi katika Msiba wa Mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Sophia Simba,Marehemu  Leeford Simba.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,Ndg. Ramadhani Madabida.
Mama wa Marehemu Leeford Simba,Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Sophia Simba akiwa pamoja na Rais Mstaafu,Mh. Benjamin Mkapa,Mama Anne Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe.Sophia Simba akieleza jambo kwa Mh. Rais Kikwete
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe. Pindi Chana akitoa salamu za pole kwa niaba ya Wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake (UWT),Asha Makame akitoa salamu za pole kwa niaba ya Umoja wa Wanawake Tanzania.
Mh. Lukuvi nae alipata nafasi ya kutoa salamu hizo kwa niaba ya Serikali.

Mh. Juma Kapuya kwa niaba ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa. Dar es Salaam Yetu

No comments: