ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 4, 2014

TASWIRA RAIS KIKWETE ALIPOKAGUA VIKOSI VYA MAKOMANDOO WA JESHI

1
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando

   ARIDHISHWA NA UTIMAMU WA VIKOSI HIVYO

  • AAHIDI TATIZO LA MAJI KUPATIWA UFUMBUZI NDANI YA MWAKA 2014
  • KIKOSI CHA UHANDISI WA MEDANI CHAAHIDIWA VIFAA ZAIDI ILI KUPAMBANA NA MAJANGA NCHINI
  • AAGIZA JWTZ KUBUNI MIKAKATI YA KUONDOKANA NA MAKAZI YA MUDA
Ziara hiyo ya siku moja ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.
(Na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT)
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taarifa ya Utawala na Utendaji kivita kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Komando wakati wa ziara yake.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye silaha na makomando kulengea shabaha.
 
 
Makomando wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila shilaha wakati wa ziara yake.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia mapambano ya kareti, taikondo na judo yaliyokuwa yakioneshwa na makomando wa JWTZ 
(Hawamo pichani).
 
 
Komando wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu alilopewa.
Kamanda wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala na Utendaji Kivita kwa (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho kutembelewa.
 
 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi Medani wa JWTZ wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli, barabara na madaraja hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na maoni kuwa kazi hizo zingehitaji muda mwingi zaidi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kuhusu moja ya  mitambo mipya inaotumiwa na Wahandisi medani kusafisha maji chumvi na baridi na kuwa maji safi na salama inayomilikiwa na Kikosi cha Uhandisi Medani.
 
Akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani.
13
 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile.

No comments: