ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 8, 2014

DUDU BAYA, Amkata Mama Yake Sikio kwa Madai ya USHIRIKINA.

Msanii mkongwe wa miondoko ya Hip Hop nchini Tanzania ajulikanae kama DUDU BAYA, anatafutwa na POLISI kwa mashtaka ya kumkata MAMA yake MKUBWA sikio kwa madai ya kishirikina. Kwa mujibu wa kituo cha redio cha mjini Dar Es Salaam CLOUDS FM mtandaoni wamesema…….. ”Kwa mujibu wa mdogo wake aitwaye Muweta alisema kuwa siku ya tukio msanii huyo alimfuata mama yake huyo nyumbani kwake na kumlaza kwenye makochi na kuanza kumkata sikio kwa kisu huku akimwambia kwanini anamroga baada ya kufanya tukio hilo alitokomea kusikojulikana”
DUDU BAYA ni msanii ambae katika fani yake ya muziki hapa nchini hiyo ni moja ya tabia zake kama anavyojulikana kwa UGOMVI, UONEVU na mambo ya ukorofi baina ya Wasanii wenzake mpaka kwa mashabiki. Kutokana na mila na desturi za kitanzania, binadamu kama hawa hawatakiwi kuwepo kwenye jamii tulivu sababu wao ndio wanahatarisha amani kwa wananchi. Kitendo tu cha kukatwa sikio kwa kisu, tena ukizingatia anaemsababishia maumivu hayo ni MWANAMKE, hiki ni kitendo cha kinyama kiasi gani?….. kuweza kufikia kufanya kitendo cha kinyama kama yeye sio bianadamu. Serikali iangalie na itilie mkazo utafutwaji na aweze kuikabiri vyombo vya sheria, sababu itakuja story nyingine kuwa kamkata sikio mwananchi mwingine.
Credit:Ngongamix

No comments: