Bodi ya wadhamini ya huduma ya Efatha, ambao ni wamiliki wa shamba la
Efatha, imemjibu katibu mkuu wa CCM, Abdulrahamn Kinana kutokana na
kauli yake kuwa atahakikisha Serikali inanyang’anya shamba hilo na
kulirejesha kwa wananchi.
Katika taarifa yake kwa umma, bodi hiyo imesema mbali na kuwa hawakubaliani na uamuzi huo, wanahoji kama mpango ni kuwapa wananchi shamba hilo, ni lini wao (Efatha) wamekoma kuwa wananchi wa Tanzania.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa baadhi ya waumini wa Efatha ni wanachama wa CCM na wengine ni
wafanyakazi wa Serikali iliyopo madarakani, hivyo nao ni wananchi wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Efatha, shamba hilo la Malonje lenye ukubwa wa hekta 15,000 lilikuwa linamilikiwa na Shirika la Maendeleo ya Mifugo (DAFCO) na kwa mujibu wa sera ya ubinafsishaji iliyopitishwa na Serikali lilikabidhiwa kwa PSRC ili waliuze.
Baada ya kutotokea mnunuzi, PSRC waliamua kutenga sehemu iliyokuwa na miundombinu, lakini bado hakutokea mnunuzi ndipo walipoamua kulikabidhi shamba hilo kwa Wizara ya Maendeleo na Mifugo na Maji mwaka 2003.
Inaongeza taarifa hiyo kuwa mwaka 2004 wizara ililikabidhi shamba hilo kwa Mamlaka ya Mkoa wa Rukwa ili kuligawa katika vipande vidogo ambavyo vingeuzika jambo ambalo pia lilishindikana.
Inazidi kufafanua mwaka 2007, Serikali iliitisha kongamano la wawekezaji na Efatha walipata mwaliko na fursa ya kuomba kununua hekta 10,000 za shamba hilo kwa ajili ya kilimo na mifugo, ombi lililokubaliwa kwa kununua shamba hilo kwa bei ya Sh600 milioni.
Wiki iliyopita akiwa ziarani mkoani Rukwa, Kinana alisema atahakikisha shamba la Efatha alilodai limepokonywa kwa nguvu, linarejeshwa kwa wananchi kwa madai kuwa Rais Kikwete alishatoa agizo la kupatiwa hekta 8,000.
via gazeti la MWANANCHI

1 comment:
Unaweza kuwa mtanzania bali zulumati.
Efatha majanga.
Post a Comment