Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe (wa tatu kushoto) na Mkuu wa
Wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo (wa pili kushoto) wakiwa pamoja na
baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom ambao baadhi yao walifundishwa na
Kanali Massawe wakati alipokuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee
jijini Dar es salaam.Kanali Massawe alifika Makao Makuu ya Vodacom kwa
shughuli za kikazi ambapo alivuta hisia za wafanyakazi waliowahi na hata
ambao hawakuwahi kupitia mikononi mwake enzi za ualimu na hivyo kuleta
hali ya furaha ikitawaliwa na utani na ukumbusho wa matuko ya Shule.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fabian Massawe akifurahia jambo na Mfanyakazi wa
Vodacom Shomary Shomary mara baada ya kukumbushana enzi za Kanali
Massawe alipokuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee wakati huo
Shomary nae akiwa ni mwanafunzi shuleni hapo. Wawili hao walikutana
wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipofika Makao Makuu ya Vodacom kwa shughuli
za Kikazi.Kanali Massawe ni mmoja wa waliowahi kuwa Walimu wakuu na
kupata heshima na sifa kubwa hapa nchini.
Ni ya kwanza kufikisha huduma za mawasiliano, Afya
Dar es Salaam, April 9, 2014 … Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu
Fabian Massawe, amezungumzia jinsi ambavyo uboreshawaji wa huduma za
mawasiliano zinavyochochea kubadili maisha ya watu kupitia kuboreka kwa
shughuli za kiuchumi na kijamii huku akipongeza maamuzi ya kampuni ya
Vodacom ya kupelekea mawasiliano kwenye kisiwa cha Goziba kilichopo Ziwa
Viktoria eneo la mkoa wa Kagera.
Kanali Masawe, ameyasema hayo wakati alipotembelea Makao Makuu ya
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom jijini Dar es salaam na kukutana na
Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wake Georgia Mutagahywa ikiwa ni
sehemu ya kutoa Shukurani kwa kufanikisha kuweka mnara wa simu katika
kisiwa cha Goziba pamoja na kusaidia ujenzi wa kituo cha afya kisiwani
humo kupitia Vodacom Foundation.
Amesema tangu Goziba ilipounganishwa kwenye mtandao wa simu za mkononi
kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika maisha ya wakazi wa kisiwa
hicho huku ikisaidiwa kwa kiwango kikubwa suala la ulinzi na usalama na
kuifungua Goziba.
“Tunawashukuru sana Vodacom, mmekuwa wa kwanza kufikisha huduma za
mawasiliano ya simu kisiwani Goziba na hivyo kuwafanya wakazi wake
kuendelea kuwakumbuka kwa namna mlivyowakomboa. “Alisema Massawe.
“Hali ya ulinzi na usalama kwenye kisiwa cha Goziba haikuwa nzuri hata
kidogo, kisiwa kilikuwa kikibaliwa na wimbi kubwa la uvamizi wa
majambazi waliokuwa wakiwavamia wavuvi na kuwapora fedha na mali zao
ikiwemo nyavu na mashine za boti huku wakikosa msaaada wowote kwani
kisiwa hakina kituo cha Polisi na hawkauwa na namna ya kuomba msaada
kutoka Bukoba kutokana na kukosa huduma za mawasiliano.”
Pamoja na kuipongeza kampuni hiyo, Kanali Masawe amesema kuwa, huduma
hizo za Mawasiliano pia zimefungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa
kisiwa hicho ambacho sasa wanawasiliana moja kwa moja na watu walioko
katika maeneo mengine ya nchi na hata nje ya Nchi hususa Nchi jirani ya
Kongo ambayo wanafanya nayo biashara ya kuuza dagaa.
“Hali hii imeimarisha shughuli za uvuvi ambao ndio msingi wa maisha ya
wanaGoziba kwani pia kwa sasa wanawasiliana na wachuuzi wa bara na hata
nje ya nchi hususan Congo DRC ambao ni wanunuzi wakubwa wa samaki na
dagaa wa kutoka Goziba na hivyo kuw ana uhakika na soko na hivyo
kupunguza usmbufu na gharama za biashara, hili ni jambo litakaloendela
kukumbukwa na kuheshimiwa na wana Goziba na mkoa kwa ujumla.”
Akizungumzia ujenzi wa kituo cha afya, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kama
ilivyo kwa huduma za mawasiliano, kisiwa cha Goziba hakikuwa na huduma
za afya na hivyo kuwafanya wakazi wake kuishi katika mazingira magumu.
Kisiwa cha Goziba kilichomo nfdanmi ya eneo la kiutawala la Wilaya ya
Muleba kipo umbali wa zaidi ya Maili 20 kutoka Bukoba ikiwachukua wakazi
wake safari isiyopungua ya saa kati ya 9 hadi 10 kufika huduma za
kijamii ikwemo afya.
“Tunawashukuru pia Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia Jamii kwa
kutusaidia kwenye ujenzi wa zahanati likiwa ni ombi la wananchi hao
wakati w ahafla ya uzinduzi wa mnara. Mngeweza kusema huduma za
mawasiliano zimetosha lakini mlikubali pia kusaidia ujenzi wa Zahanati
ya kwanza ksiwani humo ambayo inasbiriwa kwa hamu na wananachi.”
“Serikali ya Mkoa ina mpango wa kuipandisha hadhi Zahanati hiyo hiyo
kuwa kituo cha afya pindi tu ujenzi wake utakapokamilika ili kiwe na
uwezo wa kutoa huduma nyingi na bora zaidi kwa wananchi.”Aliongeza
Massawe.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kilichofanywa na Vodacom kwa watu wa Goziba
cha kuwafikishia mawasiliano na huduma za afya ni jambo lililoacha alama
kwa wakazi wa Goziba na Kagera kwa ujumla. Ni upendo wa hali ya juu wa
kampuni kwa wananchi wanaowzunguka ni vema wengine wakaona kazi hii
kubwa na nzuri ya Vodacom ili nao wajitoe kwa jamii ikiwemo za pembezoni
ambazo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii.”
Kisiwa cha Goziba bado hakina shule na kituo cha polisi.
No comments:
Post a Comment