Watuhumiwa
wa Kuchakakachua bidhaa za kampuni mbalimbali wakisindikiwa mahakamani
kujibu tuhuma zao leo mida hii katika mahakama ya mjini Moshi
Tanzania.(Picha kwa hisani ya Mtandao wa prhabari.blogspot.com)
WAELEZEWA NI WATU HATARI SANA WAIOFAA KUACHILIWA KWA DHAMAN
WANATUHUMA KILA PEMBE YA NCHI IKIWEMO DAR ES SALAAM
YAELEZWA, KONYAGI FEKI WANAZOTENGENEZA ZIMEATHIRI WATANZANIA WENGI
BAADHI
YA WAMILIKI WA MABAA WALIOHUDHURIA MAHAKAMANI HAPO WAMETOA RAI KWA
WANANCHI KUACHA KUNUNUA KONYAGI VICHOCHORONI NA BADALA YAKE KWENYE MABAA
HALALI AU MADUKANI
MAHAKAMA
ya hakimu mkazi Moshi, leo imefurika mamia ya wananchi waliokwenda
kushuhudia watuhumiwa sugu wa utengenezaji wa konyagi feki na bidhaa
nyingine mbalimbali na kuzibandika nembo za TRA ambayo inadiwa kudhuru
maelfu ya watanzania.
Hata
hivyo mahakama ya mkazi moshi imewaachia kwa dhamana watuhumiwa hao
nane ambao wanakabiliwa na tuhuma za kutumia alama za biashara za
makampuni mengine kwa nia ya kutapeli.nakujipatia pesa kinyume cha utaratibu.
Watuhumiwa
hao ni Yusuph George, Richard Leonard, Preygod Urassa, Mohamed Rashid,
Greyson Jonathan, George Kisivani, Hagai Nelson na Jackson Shayo, ambao
wanatuhumiwa kwa pamoja kwa
kutumia
kwa nia ya kutapeli alama ya biashara ya Konyagi kinyume cha sheria
huku wakijua wazi ya kuwa alama hiyo ni ya kibiashara ya halali ya
kampuni ya Tanzania Distilleries Limited.
Watuhumiwa
hawa wana kesi mbalimbali ikiwemo ile ya kutumia nyaraka za mamlaka ya
mapato nchini TRA ikiwemo mihuri yenye namba za kodi ya mapato jambo
ambalo linadaiwa kuikosesha serikali mapato mengi.
Wakili
wa serikali Julius Semali ameiambia mahakama ya mkazi Moshi kuwa
watuhumiwa hao ni hatari na kwamba wanakabiliwa na kesi za namna hiyo
maeneo mbalimbali hapa nchini.
Singida
wana kesi ya namna hii na ambayo itaendelea tena Aprili 30, 2014,
Ilala wanatafutwa na polisi kwa kukutwa na nyaraka za TRA wakati Arusha
wanatafutwa kwa kukiuka dhamana na kutoroka mwaka 2012.
Pamoja
na kupewa dhamana kwenye kesi hiyo huko Moshi, bado hakimu aliamuru
warudishwe rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Kesi
hii imevutia wammia ya wakazi ambapo miongoni mwao ambao ni
wafanyabiashara za mabaa wametoa wito kwa wananchi kuepuka kunywa
konyagi vichochoroni kutokana na madhara ambayo wameshapata watu wengi.
1 comment:
Nchi ya ajabu sana hiyo.Vipi vigogo wanaonufaika na madawa ya kulevya hawashikiki?
Post a Comment