HAPA MOJA YA BASI HILO LIKIWA KWENYE KITUO CHA MAFUTA CHA SHABIBY MKOANI DODOMA WIKI ILIYOPITA KABLA YA KUANZA SAFARI
HAPA BASI HIZO KWA NDANI KAMA ZINAVYOONEKANA
MABASI HAYO YAKIWA YAMEJIPANGA KWENYE YADI YA SHABIBY DODOMA MJINI KWA HATUA ZA MWISHO KABLA YA KUANZA SAFARI ZAKE.
BW. LIVINGSTONE MKOI AKIKAGUA KAGUA MABASI HAYO BAADA YA KUPEWA MWALIKO WAHESHIMA NA MH SHABIBY KWENYE UZINDUZI WA MABASI HAYO.
MWANDISHI HUYO AKIPIGA PICHA KAMA KUMBUKUMBU NDANI YA MABASI HAYO YA KISASA.
Na Sakina Shabani -Dodoma
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mabasi mapya yaendayo kasi ya ajabu yliyoshushwa na kampuni ya Shabiby Line yamezidi kuwa gumzo kutokana na wananchi wengi kuyakimbilia huku wakiponda mabasi mengine.
Habari toka Mkoani Dodoma ndiko makao makuu ya kampuni hiyo ukiacha Gairo zinasema kuwa wananchi wengi kwa sasa wamekuwa wakitaka kupanda mabasi hayo kwa ajili ya kujihakikishia usalama wao na kila siku ya mungu mabasi hayo hujaa siti zake mapema.
Akiongea na Xdeejayz meneja wa Kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Saidi alisema" Dada unajua haya mabasi ni mapya hivyo wananchi wengi wanahitaji kusafiri salama na haraka hivyo kwa siku mabasi yote hujaa hali inayowafanya abiria kubuku safari siku mbili kabla kwa kuhofu kukosa nafasi ndani mabasi hayo" Alisema
Hata hivyo pongezi za dhati zimfikie Mbgunge wa Jimbo la Gairo Mh' Ahmed Shabiby kwa kuonesha upendo kwa watanzania kwa kuwaondolea adha za usafiri kwani mabasi hayo mapya 26 yameanza safari wiki iliyopita na lengo lake ni kabla ya mwaka huu kumalizika atashusha mengine kama haya kwa ajili kukidhi haja ya usafiri mikoa yote Tanzania. CREDIT:XDEEJAYZ
1 comment:
hongera shabiby kwa mabasi mazuri. safari za mikoa zinakuwa very comfortable ukipanda shabiby. ila sometimes jaribu kuleta yaliyo imara zaidi maana kuna mengine mmh yako m-china sana!
Post a Comment