Mh:
Waziri wa Maji Prof.Maghembe akiwa ameambatana na Mbunge wa Iramba
Mh:Mwigulu Nchemba wakitoka kwenye Tanki Kubwa la Kutunzia maji ndani ya
Kijiji cha Nang'uli.
Waziri
wa Maji Mh:Maghembe akizindua Mradi Mkubwa wa Maji Kijiji cha Nang'uli
Jimbo la Iramba hii leo,Kulia ni Mh:Mwigulu Nchemba akishuhudia tendo
kubwa la Maendeleo ndani ya Jimbo lake.
Hatimaye
Wananchi wa Kijiji cha Nang'uli na Vijiji Vya Jilani wamepata Mkombozi
wa Maji,Mh:Mwigulu Nchemba akimtwisha Ndoo Mama wa
Kijijini hapo
kuashiria Wamepata Mkombozi wa Maji.
Wananchi
wakiwa na Furaha mara baada ya Kukabidhiwa Mradi wa Maji Kijiji cha
Nang'uli hii leo.Wananchi wameunda Uongozi wao unaosimamia Uuzaji wa
Maji kwenye Chanzo hiki,Ndoo Moja inauzwa Sh.25 tu.Mh:Mwigulu Nchemba akipokelewa na Wananchi wa Kata ya Kinapanda hii leo.Wananchi wa Kinapanda wakifuatilia Mkutano kuhusu Maji yatakavyoanza kupatikana Mapema kabla ya Mwaka huu Kuisha.
Mh:Mwigulu
Nchemba akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kinapanda kuwaeleza namna
anavyoanza kutimiza ahadi yake ya Maji kwenye Kata hiyo,Mh:Mwigulu
Nchemba amemleta Mh:Waziri wa Maji kwaajili ya Kutoa kauli yake kuhusu
hatma ya Maji ndani ya Kata ya Kinampanda.Waziri Maghembe ameahidi kuwa
Kufikia Mwezi wa 12 Mwaka huu,Makao makuu ya Kata ya Kinampanda yatakuwa
na Maji ya Kutosha na Wataanza Kusambaza Maji vijiji vya Jilani.Mh:Maghembe
akisalimiana na Wananchi wa Ulemo-Iramba wakati akiwasili kwenye
Mkutano wa Kuzungumza nao kuhusiana na Upatikanaji wa Maji ndani ya Kata
yao na namna Serikali Ilivyojipanga kusambaza Maji Vijijini.
Viongozi
wakibadilishana Mawazo,Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh:Yahya
Nawanda,Katikati ni Waziri wa Maji Mh:Maghembe na Mwisho Kulia ni
Mh:Mwigulu Nchemba Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba.
Mh:Mwigulu
Nchemba akimshukuru sana Waziri wa Maji kwa Kufanikisha Miradi ya Maji
katika Jimbo lake hasa Kata ya Ulemo,Kinampanda,Kiomboi,Ndago na Kijiji
cha Nang'uli.
Waziri
wa Maji Prof,Maghembe akizungumza na Wananchi wa Ulemo kuhusiana na
Utekelezaji wa Mradi wa Maji ndani ya Kata yao.Waziri ameahidi kuwa
Serikali imetenga zaidi ya Sh.800 Milioni kwaajili ya Kusambaza Maji
kata ya Ulemo.Zoezi hilo limekabidhiwa kwa Mhandisi wa Mkoa/Wilaya na
Ofisi ya Mkurugenzi tayari kwaajili ya Kuanza kutimizwa."Maji safiiiiiiiiiiiiiiii"
Wananchi wa Kijiji cha Nang'uli wakishangilia Kupata Maji ndani ya Kijiji Chao.
Waziri
wa Maji Mh:Maghembe hii leo amefanya ziara ya Kukagua Maendeleo ya
Utekelezaji wa Miradi ya Maji Jimbo la Iramba,Katika hatua hiyo
Mh:Maghembe amefungua Rasmi Mradi wa Maji wa Kijiji cha Nang'uli na
Kuukabidhi kwa Wananchi Waanze kuutumia.
Mbali
na Kufungua Mradi huo,Akiwa ameambatana na Mbunge wa Iramba Mh:Mwigulu
Nchemba,Prof Maghembe amezungumza na Wananchi wa Kata ya Kinampanda na
Ulemo kuhusu Mpango wa Kusambaza Maji ndani ya Vijiji vya Kata hizo pia
Kuchimba Visima Vikubwa vya Maji ilikuwezesha Upatikanaji wa Maji ya
Uhakika kwa Wananchi.
Maghembe
amesema "Serikali imetenga Fedha zaidi ya Milioni 80 kwa Kijiji cha
Uleo kwaajili ya Kusambaza Maji,Pia Imetenga fedha kwaajili ya Kuchimba
Kisima Kikubwa kata ya Kinampanda kwaajili ya Kupata Maji mengi na
hatimaye yasambazwe Vijiji mbalimbali ndnai ya Kata hiyo,Mh:Maghembe
amewasihi Wananchi kuunga mkono Juhudi hizo zinazofanywa na serikali ya
CCM,Pia amempigia Chepuo Mh:Mwigulu Nchemba kuwa amekuwa Moja ya Wabunge
wanaofuatilia sana Mahitaji ya Wananchi wake hasa Maji.
Mbali
na Mh:Maghembe,Mbunge wa Iramba N/Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba
akizungumza na Wananchi wa Kinampanda amesema atahakikisha anatimiza
kile alichokiahidi kabla hajakwenda kuomba ridhaa ya kuwaongoza tena
wananchi wa Iramba,"Niliwaahidi maji hapa,nitahakikisha Maji
yanapatikana Kabla ya Mwaka 2014 kumalizika,Nashukuru Waziri ametoa
kauli kuwa Fedha zipo kilichobaki ni utekelezaji tu,Mkataba wangu na
Nyie Wananchi ni Maendeleo tu,Nikishindwa Kuwaletea Maendeleo ni
Kutowatendea haki".Mwigulu.
Wakizungumza
kwa Nyakati tofauti Wananchi wa Nang'uli na Ulemo wametoa Pongezi zao
za dhati kwa Mbunge wao Mwigulu Nchemba kwa Kuwapelekea Maji,Wamesema
Wanaona Kazi anayoifanya kwenye Umeme,Elimu,Afya na sasa amewapelekea
Maji,Hivyo hawahitaji Kumpoteza kiongozi huyo kwakuwa ni Mchapakazi
sana.
Habari/Maelezo na Sanga Festo
No comments:
Post a Comment