ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 6, 2014

MCHANGO WA "HOLLYWOOD" KATIKA KUTOA ELIMU KWA JAMII KUHUSIANA NA UHALIFU MTANDAO.

Unapozungumzia vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na wacheza Filamu Televishen na Redio Hollywood imekua mstari wa mbele katika kutoa elimu ya kina kuhusiana na makosa mtandao jinsi yanavyo tendwa na namna ya kutambua na kujikinga.

Kumekua na kampeni endelevu Kupitia tamthilia mbali mbali pamoja na muvi zinazotengenezwa marekani kuhakiki jamii inatambua aina mpya ya makosa mtandao yanaingizwa katika vipengele mbali mbali ndani ya Filamu zinazotengenezwa.

Baadhi ya Mifano hai ni kutoka katika tamthilia ya "The event" episode ya 3 Ilipo toa elimu kuhusiana na Neno la siri "Password", Tamthilia ya "Nikita" Imekua ikitoa elimu takriban katika kila "episode" iliyokua inatolewa huku katika "episode" yake ya Kwanza katika "season" ya mwisho - kama inavyo onekana kwenye video hapo hapo chini, elimu dhini ya teknologia mpya inayo tumiwa na wahalifu ambayo kwa sasa imeonyesha kushika kasi ambapo mhalifu anauwezo wa kufatilia mazungumzo yako yote ya simu na kurekodi, pia ilionyesha camera zilizo endelea kushika kasi ambazo mhusika anavyaa katika mboni ya macho ambapo ni vigumu kutambua.

Aidha Tamthilia nyingine nyingi zimekua ziki endelea kutoa elimu mbali mbali za maswala ya uhalifu mtandao katika vipengele mbali mbali kwa malengo ya kuhabarisha jamii kupitia tasnia ya filamu maswala ya ulinzi mtandao.

"Imefika wakati sasa kwa Tanzania kuihusisha tasnia ya filamu nchini kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na maswala ya uhalifu mtandao, jinsi ya kugundua na kukabiliana nayo ili kuongeza wigo wa uelewa kwa jamii nchini kwani inaaminika kupitia filamu darasa linaeleweka zaidi kwani wana filamu wananafasi kubwa sana katika kutoa elimu mbali mbali katika jamii." - Yusuph Kileo.

Vita dhidi ya uhalifu mtandao si vita ya kundi fulani la watu au aina fulani ya watu bali ni swala linalo anzia katika ngazi ya mtu binafsi na kuonganisha nguvu ili kuhakiki taifa na dunia kwa ujumla inakua salama kimtandao.

"Kwa kuzingatia Hili natoa wito kwa jamii ya kitanzania kutambua hali hii ya uhalifu mtandao na kuhakiki jitihada za dhati zinachukuliwa mapema bila ya kungoja hali kuwa mbaya kiasi cha kuwa na ugumu kupata suluhu ya jinsi ya kukabili uhalifu mtandao nchini "

Picha hapo inaonyesha Sehemu ya Kipande Kutoka katika Filamu ya "Italian Job" ambapo filamu hiyo nzima ilikua imejikita katika kutoa elimu ya maswala ya uhalifu mtandao.

1 comment:

Anonymous said...

wao ndo wamanzo kusambaza maovu yote yanayotokea duniani wanadhani watu hawajui wawadanganye hao hao wadanganyika wenginewe lakini si wote ndo maana nasema shule ni muhimu sana hata kama unapiga boxi lakini angalia shule itakukomboa sana na kujua mambo yanakwendaje hapa duniani na kuwa mstaarabu wa kujua kuzungumza na watu na kuishi na watu si kwa chuki na majungu