Kenny Mwangoka akiendesha gari hilo ambalo bodi lake limetengenezwa kwa mbao |
Kenny Mwangoka akifungua mlango wa nyuma wa gari hilo akionesha umadhubuti wa bori lake |
Mwanahabari huyu Oliva Motto wa Star TV hakuamini kama kilichounda bodi ya gari hilo ni mbao mpaka alipogusa na kujiridhisha |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Peter Tweve akimpongeza Mwangoka kwa ubinifu huo |
Na Francis Godwin, Iringa
Amini
usiamin. Bodi la gari hili aina ya Hiace lenye namba za usajili T921
BME limetengenezwa kwa mbao aina ya mlingoti na pine. Linamilikiwa na mvunaji na mfanyabishara wa mbao wa Nyololo, Mafinga, mkoani Iringa Bw.Kenny Mwangoka.
Mwangoka alilinunua gari hilo lililokuwa linamilikiwa na mission ya
kanisa katoliki Mafinga baada ya kupata ajali na kuharibika
vibaya. Jitihada zake za kulifufua gari hilo kwa kuvisha bodi mpya
hazikuzaa matunda na ndipo alipotumia ubunifu huu.
"Mimi mwenyewe ni fundi wa magari, kwahiyo kazi ya kuunda na kuvisha
bodi hili la mbao nilifanya mwenyewe," anasema, na kuongeza kuwa baada
ya matengenezo hayo gari hilo limekuwa kivutio kikubwa sehemu mbalimbali
anazopita nalo.
"Sasa nalitumia kuhamasisha utalii, hasa utalii wa mazingira nikiwa na
maana kwamba tukiyatunza mazingira yatatufaa kwa mambo mengi ikiwa ni
pamoja na matengenezo ya magari kama hili langu," anasema, na kuongeza
kuwa atalipeleka kwenye maonesho ya nanenane mwaka huu kama moja ya
njia za kuhamasisha upandaji wa miti
1 comment:
this matatu should not be on the road - dangerous
Post a Comment