Balozi Tuvako Manongi.
Balozi wa kudumu wa Tanzania umoja wa mataifa Mhe, Tuvako Manongi siku ya Ijumaa atakabidhi bendera kwa timu ya mpira wa miguu ya New York katika chakula cha jioni atakachowaandalia maalumu cha kuwatakia kheri kwenye mechi ya timu hiyo itakaposhuka dimbani siku ya Jumamosi May 24, 2014 kwa mpambano unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa kabumbu utakaochezewa Capitol Heights, Maryland katika uwanja wa Walker Mills Park.
Lengo la Ghafla hiyo nikuwatia nguvu na
kuwapa ari mpya wachezaji na viongozi watakaoandamana na timu kuelekea DC kwenye mechi inayosubiliwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka wa DMV na vitongoji vyake. Mechi hiyo ambyo wachezaji wameishaanza kutambiana itakuwa ni katika moja ya shamra shamra za Memorial weekend ambayo kwa mara ya kwanza katika historia inafanyika DMV. Sherehe hivi miaka ya nyuma zimekuwa zikisherehekewa Columbus, Ohio na lengo kubwa ilikuwa kuwakutanisha Watanzania lika mbambali kutoka kila kona ya Marekani kucheza michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa kikapu, miguu na baadae kuruka rhumba mpaka asubuhi.

Balozi Tuvako Manongi alipoongea na VIJIMAMBO alisema anafurahi sana kuona timu ya mpira ya New York ikifanya vizuri na anamatumaini itarudi na kombe litakalotokana na ushindi mnono wa vijana wake dhidi ya timu ya DMV.
Timu ya New York ipo kwenye mazoezi makali kujiandaa na matanange wao na timu ya DMV hapo siku ya Jumamosi. Kocha wa New York amesema vijana wake wapo fiti na tayari kwa mpambano, ushindi kwetu lazima, kufungwa mwiko. Wembe tulioutumia kumnyoa Boston ndio huo huo utakaogeuzwa upande wa pili kuinyoa timu ya DMV.
No comments:
Post a Comment