ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 4, 2014

CDA yabomoa nyumba zaidi ya 65 Mlimwa kusini manispaa ya Dodoma

 Tingatinga la Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] likibomoa moja ya nyumba zilizopo katika hifadhi ya Barabara inayotarajiwa kuanza kujengwa havi karibuni, ambapo zaidi ya nyumba 65 zilibomolewa katika eneo hilo la mlamwa kusini.
 Wanawake wa mtaa wa Mlimwa wakimsaidia Mwenzao aiyezilai baada ya Tingatinga la CDA kufika kwa ajili ya kubomoa nyumba yake kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Barabara, zoezi hilo lilifanyika Jana ambapo nyumba zaidi ya 65 zilibomolewa na kuacha familia zaidi ya 150 zikikosa makazi.
 Mwenyekiti wa mtaa huo Zubeda Haji akielekeza jambo wakati wa ubomoaji huo.
 Wananchi wa Mlimwa waking'oa mabati muda mfupi kabla ya Tinga tinga la CDA kufika na kuibomoa nyumba hiyo ili kupisha hifadhi ya Barabara
  Bibi huyu mkazi wa Mlimwa Kusini ambaye hakufahamika jina lake akiwa hajui la kufanya baada ya nyumba yake aliyokuwa akiishi iliyojengwa kwa mtindo wa Tembe huku akiachwa na vyombo vyake alivyoweka kwenye shamba la mahindi baada ya CDA kufanya uvunjaji huo kwa nyumba zote zilizopo katika hifadhi ya Barabara.
Wananchi wa Mlimwa kusini wakiwa katika hekaheka ya kuhamisha mizigo yao na kukimbia nyumba zao baada ya kupata taarifa za ujio wa Tinga tinga la CDA kwa ajili ya kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara.

PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJA BLOG

6 comments:

Anonymous said...

INASIKITISHA SAAANA JAMANI,HII SERIKALI YETU DAH EEH MWENYEZI MUNGU WAPE NGUVU VIUMBE WAKO WALIOADHILIKA NA UTARABIBU HUWO. JAMANI HALAFU NASIKIA WALIPWI SASA WATAISHIJE? KAZI ZENYEWE HAKUNA TANZANIA. HUU NI UONEVU MKUBWA.YANI TANZANIA UKIWA MASKINI HAITOSHI LAZIMA WAKUFANYE UWE MASKINI WA KUTUPWA. WATCH...HIYO BARABARA HAITAJENGWA LEO WALA KESHO NI WIZI NA UONEVU TU.MUNGU YUPO INSHALAAH

Anonymous said...

NALAUMU SERIKALI YETU KWA SABABU KAMA WALIJUA WATAJENGA BARABARA KWA NINI WANAACHIA WANANCHI WANAJENGA WANGEWAKATAZA NA KUWAAMBIA HILO NI ENEO LA SERIKALI WANAMPANGO WA KUJENGA BARABARA AU CHOCHOTE KWA KWELI NI AIBU SANA KWA NCHI YETU KUWABOMOLEA WANANCHI MAHALI AMBAPO WANAISHI WAMEJIKAMUA HUKU NA KULE ILI WAWEZE KUPATA MAKAZI YA KUISHI HALAFU WANAAMBULIA SIFURI HATA KIFUTA MACHOZI KWELI NI DEMOKRASI HIYO SIAMINI

Anonymous said...

INAUMA SAANA, HAWAKUJENGA BILA KUNUNUA VIWANJA NA KUPEWA VIBARI NA SERIKALI YA MITAA SASA KWANINI HAWALIPWI????UONEVU TU KWA VILE WATANZANIA WATULIVU ILA UTULIVU UNAISHAGA NA UKIISHA WATAJUTA.

Anonymous said...

INAUMA SAANA, HAWAKUJENGA BILA KUNUNUA VIWANJA NA KUPEWA VIBARI NA SERIKALI YA MITAA SASA KWANINI HAWALIPWI????UONEVU TU KWA VILE WATANZANIA WATULIVU ILA UTULIVU UNAISHAGA NA UKIISHA WATAJUTA.

Anonymous said...

MSIJE KUSHANGAA RIDHIWANI ANAGOMBEA URAISI..YALE YALE YA BABA BUSH NA MTOTO BUSH.

Anonymous said...

GOD BLESS TANZANIA CITIZENS.