Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa Jimbo la Sikonge Said Mkumba wakiwasomea wananchi wa kijiji cha Lukula maeneo yatakayopata umeme mwaka huu katika wilaya ya Sikonge.
Mbunge wa Jimbo la Sikonge Said Mkumba akihutubia wananchi wa kijiji cha Lukula kata ya Mgambo na kuwaambia wale wote waliodhulumu wakulima wanatakiwa kuchukuliwa hatua na pia alisisitiza sheria zingatiwe za wanasiasa kutojihusisha na masuala ya vyama vya ushirika.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipitia taarifa mbali mbali kabla ya kuhutubia wakazi wa kata ya Mgambo,Katibu Mkuu wa CCM amehuzunishwa sana na baadhi ya viongozi wa Serikali kutofika kwa wananchi na kujua matatizo yao badala yake wamesababisha wananchi kuumia sana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya ujenzi wa jengo la upasuaji na Dk.Silvanus Kabutura Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Kata ya Kitunda wilayani Sikonge,Daktari Kabutura alimueleza Katibu Mkuu wa CCM changamoto kubwa uhaba wa maji katika kituo hicho.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kukagua jengo la upasuaji la kituo cha afya cha Kitunda wilayani Sikonge mkoani Tabora ambalo limechelewa kukamilika kwa zaidi ya mwaka mmoja na huku Wizara ya Afya kushindwa kuchukua hatua mpaka sasa .
No comments:
Post a Comment