ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 4, 2014

MAMBA ALIYEKUWA AKIISHI KWENYE MAKAZI YA WATU KINONDONI JIJINI DAR AUWAWA

 Yule Mamba aliyekuwa akiishi kwenye makazi ya watu Kinondoni Block 41, jijini Dar es Salaam hatimaye leo May 4, 2014 ameuliwa kwa kupigwa na risasi zipatazo nne. Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio alisema kuwa Mamba huyo amekuwa akiishi kwa muda mrefu licha ya Wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika.
"Leo ameuwawa Mamba ambaye alikuwa akitulaza kwa hofu maana alitokea kujichanganya kwenye makazi ya watu ndipo watu walipomshambulia na baadae ilibidi tupate msaada wa jirani yetu ambaye alikuwa na bastola  na kufanikiwa kumpiga risasi nne na kumuua. Picha zote na EMMA Mdau wa Kajunason Blog akishirikiana na Erick Mgema.
Mamba akiwa amewekwa juu ya gogo ili wananchi wamwangalie vizuri katika kituo cha Osterbay jijini Dar.
Mamba alikuwa amekomaa kukadiliwa anaumri wa miaka mitano...

1 comment:

Anonymous said...

Serekali ya Tanzania, Rais JK - You have failed the residents of block 41. Mamba anaishi kwenye bwawa for years juu ya mifereji kuelekezwa hapo. Mbu za matende zimejaa humo. FYI kuna other crocodiles in that stagnant water. Serekali Plse look into this.