Msanii nyota wa kike wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khadija Shaban
maarufu kama ‘Keisha’ amejifungua mtoto wa
kiume siku ya Jumatatu (Mei
5) katika hospitali ya Mount Mkombozi Kinondoni.
Akizungumza na Bongo5 leo Keisha,amesema anashukuru Mungu amejifungua
salama na mtoto anaendelea vizuri. “Nimejifungua mtoto mwingine wa kiume
katika hospitali ya Mount Mkombozi Kinondoni. Namshukuru Mungu
nimejifungua salama na mtoto anaendelea vizuri,” amesema.
No comments:
Post a Comment