Okwi alisaini mkataba wa dola 100,000 ambazo ni zaidi ya Sh160 milioni lakini Yanga ilimpa kianzio cha dola 60,000 (Sh96 milioni) hivyo sasa anadai dola 40,000 (Sh64 milioni) na hapo ndipo sekeseke lilipo.
Okwi tulimpa mkataba wa miaka miwili na nusu huku tukikubaliana tufuatilie hati ya uhamisho wake ili aichezee Yanga, ila ilichelewa na akakosa baadhi ya mechi, lakini baadaye akajitoa katika timu bila kuutaarifu uongozi akitaka amaliziwe fedha zake ndiyo aendelee kuichezea Yanga.
kauli ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji, kumhusu nyota wao, Emmanuel Okwi? Sasa imepata majibu kutoka kwa Mwanasheria wa mchezaji huyo, Edgar Aggaba, aliyesema: “Acheni mchezo, sisi tunataka fedha zetu tu.”
Ishu ni fupi sana, Manji wakati anazungumza na waandishi wa habari Jumapili iliyopita alisema mambo mengi, lakini aligusia sakata la Okwi na klabu hiyo ambapo alisema: “Okwi tulimpa mkataba wa miaka miwili na nusu huku tukikubaliana tufuatilie hati ya uhamisho wake ili aichezee Yanga, ila ilichelewa na akakosa baadhi ya mechi, lakini baadaye akajitoa katika timu bila kuutaarifu uongozi akitaka amaliziwe fedha zake ndiyo aendelee kuichezea Yanga.
“Sasa kutokana na hali hiyo ya kushindwa kuichezea Yanga baadhi ya mechi, inabidi achague ama kuongeza mkataba wake hadi miaka mitatu au sehemu ya fedha anayodai ikatwe.”
Okwi alisaini mkataba wa dola 100,000 ambazo ni zaidi ya Sh160 milioni lakini Yanga ilimpa kianzio cha dola 60,000 (Sh96 milioni) hivyo sasa anadai dola 40,000 (Sh64 milioni) na hapo ndipo sekeseke lilipo.
Lakini akizungumza na Mwanaspoti akiwa Uganda, Aggaba alisema ameisikia kauli ya Manji kuhusiana na mteja wake Okwi, hata hivyo akasisitiza kwamba amekubaliana na mchezaji huyo kukaa meza moja na Yanga kuzungumza juu ya kukosa mechi sita, lakini kwanza alipwe fedha zilizobaki.
Aggaba alisema Yanga inatakiwa kumlipa kwanza Okwi fedha zake ambazo ahadi ya kumlipa mapema siku chache baada ya kutua nchini ndiyo iliyotangulia vinginevyo watakuwa na uamuzi mwingine juu ya mkataba wa mchezaji huyo.
Mwanasheria huyo alisema atazungumza na Okwi ambaye leo (Ijumaa) asubuhi alikuwa safarini na kikosi cha Uganda ‘The Cranes’ kuelekea Madagascar kucheza mechi ya kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Alisema endapo Yanga itashindwa kumlipa fedha zake hadi Juni 30 mwaka huu wataanza mchakato wa kuvunja mkataba.
“Hapa kuna mambo mawili, la kwanza ni Okwi kulipwa fedha zake za usajili, hilo ndiyo lililotangulia.
Pia ni Yanga kutaka wafidiwe baada ya Okwi kukosa mechi za mwanzo, kama wanataka tuzungumze hakuna shida, lakini nafikiri kwanza wanatakiwa kukamilisha jambo la kwanza ambalo ni malipo ya mchezaji ambayo tulikubaliana wakati anasajiliwa kuwa akifika Tanzania atalipwa haraka,” alisema Aggaba.
“Yanga wanatakiwa kukumbuka kwamba Okwi hakujizuia kuichezea Yanga, ni matatizo ya huko Tanzania kutojua kanuni ndiyo yaliyomfanya ashindwe kuichezea timu, nitazungumza na Okwi akirudi Madagascar na kama Yanga hawatamlipa mpaka kufika mwisho wa mwezi Juni mwaka huu tutaangalia la kufanya likiwamo la kuvunja mkataba.”
Okwi alikosa mechi tatu za kwanza za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara msimu uliomalizika hivi karibuni dhidi ya Ashanti United, Coastal Union na Mbeya City pia ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine de Domoni ya Comoro kutoka na utata wa usajili wake.
Pia alikosa mechi tano za mwisho za ligi ambazo ni dhidi ya Simba, JKT Oljoro, JKT Ruvu, Kagera Sugar na dhidi ya Rhino Rangers baada ya kugoma akishinikiza kulipwa chake.
Yanga ilimsajili Okwi kutoka SC Villa ya Uganda kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
No comments:
Post a Comment