ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 16, 2014

Je, Diamond awa “GHOST” kufanya Show USIKU wa LEO Billicanas DAR na Kesho) DIAMOND PLATNUMZ LONDON SHOW 2014 PROMO VIDEO


 Je, Diamond awa “GHOST” kufanya Show USIKU wa LEO Billicanas DAR na Kesho 
‘Mi Casa’ Band kutoka SOUTH AFRICA inatua jijini Leo kwa ajili ya show ya ‘MTV Road To Mama’ itakayofanyika Leo hii Club Billicanas kuwapongeza wasanii walioingia kwenye nomination ya MTV Afrika. Show hii ambayo imeandaliwa na MTV wenyewe ni kwa ajili ya kusherehekea Nomination ya wasanii Wa
East Africa ambao baadhi yao watanya show usiku huo. Double MTV Awards Nominee and a BET Awards Nominee “Diamond Platnumz” ambae nae anatarajiwa kuingia nchini Leo kutoka nchini UK alipokua anafanya Video ya nyimbo yake mpya.


Cha kushangaza ni kwamba ‘Diamond Platnumz’ akiwa na swaiba wake ‘Ommy Dimpoz’ ambae wamekuwa safari moja mjini London, inasadikiwa pia kuwa Saturday 17 May 2014 ametangaza show mjini hapo chini ya promoter BONGOUK na Club MALIBU sasa sijui atakua GHOST??? kuweza kupatikana katika miji miwili kwa wakati mmoja yaani Friday 16th May 2014 Bilicanas ambayo ni Leo na Saturday 17th May 2014 mjini London ambayo ni kesho na ukizingatia yupo mjini London Tayari, ukweli kabisa maana kama Diamond ataingia Leo kwa ajili ya show sidhani kama ataweza kuondoka usiku huu au alfajiri kuweza kurudi mjini London tena kwa ajili ya show ya mashabiki wake wa nchini humo. Je kuna utapeli unaofanyika kati ya promoters hawa yani MTV na BONGOUK wakishirikiana na Club MALIBU ya nchini Uingereza?

Katika Video clip iliyowekwa kwenye mtandao wa “JestinaGeorge blog” ambao wanamuziki hao ‘Ommy Dimpoz’ na ‘Diamond’ wakiwahamasisha watu kuwepo katika show hiyo inayofanyika ‘Oasis Banquette’ maeneo ya ‘East London’ wasanii hao binafsi wamekuwa wakipromote show hiyo na kuonyesha uwepo wao mjini London na hawakuweza kuzungumzia chochote kuhusiana na show ya MTV party inayofanyika Leo mjini Dar.

Kutokana na Source ya MTV ambayo imetakaa jina lake lisitajwe amezungumza kuwa Diamond yupo Dar tayari kwa ajili ya show hiyo ya MTV na kusema kuwa akimaliza show hiyo siku ya leo atarudi UK kiasi ambacho kutokana na kutokuwepo na ndege ya “British Airways” mjini Dar ambayo zamani ilikua inafanya safari zake kuanzia Dar asubuhi saa 1 (7am East African Time) na kutua mjini London saa 11 jioni (5pm || 1700hrs London Time) haifanyi safari zake hizo tena kwahiyo itakuwa ngumu sana kwa msanii huyo kuweza kufanikiwa kurudi na kufanya show kwa ajili ya wananchi wa mjini London.

Source ya nchini London imesema kuwa msanii huyo atageuza na “Turkish Airline” ambayo ataondoka nayo Dar Saturday saa 11 alfajiri (5am EAT) na kuingia London saa 10 jioni Jumamosi hiyo hiyo (4pm || 1600hrs London Time). Big Up Diamond tupo nyuma yako.

Sasa huyu ndio maana akaitwa STAR, superstar “Diamond Platnumz Beybe” sababu anaroll kama star, “2 Days 2 Continent”, 3 Big Awards Nomination (BET, MTV, CORA) .Akiwa anaongoza nyumbani na kuvunja record ya “7 Awards winning”
:Credit:Gongamix.

No comments: