Mwandishi: Akwisuss Chabruma
Student University of Dar es Salaam, College of social science ( CoSS), 0616438250
UTANGULIZI
✍🏼Katika historia ya siasa za Tanzania, wapo viongozi ambao mchango wao unaendelea kukumbukwa hata baada ya kuondoka duniani..✍🏼
Miongoni mwa viongozi hao ni marehemu Selina (Celina) Ompeshi Kombani, mwanamke jasiri, mchapakazi na kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Wilaya ya Ulanga na Taifa la Tanzania kwa ujumla... ✍🏼
Kwa miaka mingi ya utumishi wake, Selina Kombani alijijengea heshima kubwa kutokana na uadilifu, bidii na uwezo wake wa kusimamia masuala ya wananchi. ... ✍🏼
Selina Kombani alikuwa mfano wa mwanamke aliyethibitisha kuwa uongozi si suala la jinsia bali ni uwezo, maono na uzalendo... ✍🏼
HISTORIA YAKE KWA UFUPI
🍼Selina Ompeshi Kombani alizaliwa tarehe 19 Juni 1959 katika Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro.
👨🏼🎓Alipata elimu yake ya juu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe ambako alihitimu shahada zake kabla ya kuingia kikamilifu katika utumishi wa umma na siasa.
🟩Selina Kombani alikuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki mwaka 2005, nafasi aliyoiendelea kuitumikia hadi mwaka 2015... ✍🏼
SAFARI YAKE YA UONGOZI
Baada ya kuingia Bungeni, uwezo wake wa kiuongozi ulionekana mapema na kuaminiwa na Rais Jakaya Kikwete ( Raisi wa Tanzania awamu ya nne)kushika nyadhifa mbalimbali serikalini.
Miongoni mwa nafasi alizowahi kushika ni:
1.Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (2006–2008)
2.Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (2008–2010)
3.Waziri wa Katiba na Sheria (2010–2012)
4.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (2012–2015)
🫂Katika nafasi hizo, alijulikana kwa kusimamia uwajibikaji, nidhamu katika utumishi wa umma na kuhimiza utoaji bora wa huduma kwa wananchi.
MCHANGO WAKE KATIKA ULANGA
Kwa wananchi wa Ulanga, Selina Kombani alikuwa zaidi ya Mbunge. Alikuwa mlezi, mshauri na mtetezi wa maendeleo yao.
Wananchi wengi wanakumbuka kwa:
1.Kusukuma mbele maendeleo ya miundombinu ya barabara.
2.Kusaidia wanafunzi kupata ada na fursa za elimu.
3.Kuwezesha vijana na wajasiriamali wadogo.
4.Kutetea huduma za afya na maendeleo ya jamii.
Mchango wake ulifanya wananchi wengi wa Ulanga kumwona kama kiongozi aliyekuwa karibu nao na aliyegusa maisha yao moja kwa moja. 😭😭
🏥URITHI WAKE KATIKA SEKTA YA AFYA
Mbali na siasa, Selina Kombani alihusika katika juhudi za kuimarisha huduma za afya, hususan katika Wilaya ya Ulanga.
Selina Kombani anatajwa kuwa ni mmoja wa viongozi waliochangia kuhamasisha ajira za wahudumu wa afya ngazi ya jamii, hatua iliyosaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa maeneo ya vijijini.... ✍🏼
🪦KIFO CHAKE NA MAOMBOLEZO YA TAIFA
Tarehe 24 Septemba 2015, Taifa la Tanzania lilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Selina Kombani. ...
Umauti ulimkuta akiwa nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu akiwa na umri wa miaka 56... ✍🏼
Kifo chake kilizua huzuni kubwa miongoni mwa wananchi wa Ulanga, viongozi wa serikali na Watanzania kwa ujumla. ... 😭😭
Katika Msiba wake watu wengi walimwelezea kama kiongozi mchapakazi, mwenye ushirikiano na aliyejitolea kwa dhati kuwatumikia wananchi wake... ✍🏼
HITIMISHO
Maisha ya Selina Kombani ni somo muhimu kwa kizazi cha sasa na kijacho. Alionyesha kuwa uongozi bora unahitaji kujitoa, kufanya kazi kwa bidii na kuweka maslahi ya wananchi mbele... ✍🏼
Ingawa ameondoka duniani, mchango wake katika maendeleo ya Ulanga na Tanzania utaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi ijayo.
Jina lake limebaki kuwa sehemu ya historia ya viongozi wanawake waliolipigania Taifa kwa moyo wote.
"Viongozi huondoka, lakini matendo yao mema huendelea kuishi katika mioyo ya watu."
@ Wewe Msomaji wangu utamkumbuka SELINA OPESHI KOMBANI kwa lipi???




No comments:
Post a Comment