Thursday, May 15, 2014

Upungufu wa nguvu za kiume unavyotibika

Dismas Lyassa 
Kwa ajili ya matatizo mbalimbali yaliyo katika jumuiya, pamoja na kwamba tendo la ndoa ni jambo la msingi kwa wale waliooana, kuna wanaume aidha hawana uwezo wa kulifanya tendo hili au wana hisia ndogo na nguvu kidogo za kutekeleza tendo hili.
HAMU ya tendo la ndoa kwa mwanadamu au mwanamke ni moja ya hisia za msingi kwa mwanadamu wa kawaida kama ilivyo njaa au usingizi.

Kwa ajili ya matatizo mbalimbali yaliyo katika jumuiya, pamoja na kwamba tendo la ndoa ni jambo la msingi kwa wale waliooana, kuna wanaume aidha hawana uwezo wa kulifanya tendo hili au wana hisia ndogo na nguvu kidogo za kutekeleza tendo hili.

Kwa kuwa hali ya kukosa hisia au nguvu za kufanya tendo la ndoa ni dhahiri zaidi kwa wanaume, matatizo yanayozungumzwa hapa chini ni kuhusu wanaume; hata hivyo wanawake kama ni tiba ambayo iko kwa ajili ya wanaume, nao wanaweza kuitumia hiyo hiyo kwa lengo la kuongeza hisia za kufanya tendo hilo.

Kwa zaidi ya miaka 13 sasa nimekuwa nikiandika kwenye magazeti na kuitwa kwenye vituo mbalimbali vya televisheni na redio kuzungumzia masuala ya ndoa, idadi ya watu ambao wamekuwa wakisoma au kufuatilia kazi zangu kwa ujumla ni wengi mno, ndani na nje ya Tanzania, baadhi yao wamekuwa wakiniuliza “Dismas unasisitiza wanandoa waelewane, sasa inakuwaje mimi mwenzi wangu hana nguvu, kwani mimi nimefuata kula…” Kuna idadi kubwa ya wanawake wanatoka nje ya ndoa kwa siri kwa sababu waume zao siyo imara.

Kwa bahati mbaya sana kuna wanaume wanafikiri tendo hili kwa wanawake siyo muhimu, wapo ambao wanafikiri kwamba wanawake wanachokifuata kwenye ndoa ni fedha au kula, ndiyo utawasikia wanaume wengine wakiwaambia wake zao “Kwani tatizo nini, mbona ndani kuna kila kitu, fedha ziko, chakula kipo, mbona wewe mwanamke huna shukrani.”

Ni kutokana na baadhi ya wasomaji kuniomba nifanyie utafiti tatizo hili, nimelazimika kuwasiliana na baadhi ya watafiti ambao wanashughulikia masuala ya nguvu za kiume na tendo la ndoa kwa jumla kutoka nchi mbalimbali zikiwamo Ujerumani, Finland, Marekani, Ufaransa na hatimaye nikapata ushirikiano mzuri na wa karibu zaidi kutoka kwa mojawapo wa mabingwa wa mfumo wa uzazi India, Dk Srinivasakumar K.P.

Niliweza kuzungumza na mtaalamu huyu wa tiba kwa kutumia vyakula mwenye elimu ya shahada ya uzamivu (PhD), na kwa bahati nzuri aliweza kuja Tanzania mara mbili kuangalia mazingira ya Tanzania na kufanyia utafiti tatizo hili la nguvu za kiume. Tangu aanze kufanyia utafiti tatizo hili ni zaidi ya miaka minne sasa, akitokea kituo chake cha kiitwacho Institute of Biology and Clinical Research (IBCR).

Katika utafiti tulibaini kuwa upungufu wa nguvu za kiume unaweza kugawanywa katika makundi matatu ambayo ni (i) umbile la mwanamume kutokuwa na uwezo wa kusimama wakati wa tendo la ndoa au wakati mwingine wowote…hali hiyo huitwa uhanithi. ii) Umbile la mwanamume kutokuwa imara kiasi kwamba wakati mwingine mwanamume anashindwa kulifanya tendo. (iii) Kadri mwanamume anavyoingia katika umri mkubwa, nguvu zake nazo zinaendelea kupungua.

Baadhi ya sababu za kuwa na tatizo la nguvu za kiume ni; msongo wa mawazo, uchovu wa mwili, ulevi kupita kiasi, kupooza mwili, ugonjwa wa kisukari, kujichua nk.

MSAADA THABITI
Mtaalamu huyo anasema ni vyema kutengeneza mchanganyiko wa vyakula maalumu ambavyo mtu anaweza kuvitumia na tatizo hilo kumalizika. Mchanganyiko wa vyakula ukitumiwa vizuri unamsaidia mwanamume kuwa imara, bila kujali ni kwa miaka mingapi amekuwa na tatizo hilo. Wengi wa wale ambao wamekuwa wakizingatia maelekezo wamekuwa wakifanikiwa. Ndugu huna sababu ya kulalamika, chukua hatua.

No comments: