Askari wa Bend kutoka JKT wakiongoza maandamano ya wanafunzi wanaosoma katika shule mbalimbali za Mkoa wa Dodoma.Maandamano yaliyoanzia Viwanja vya kumbukumbu ya Mwl. Nyerere hadi Uwanja wa Jamhuri.
Kikosi cha Bendi ya Shule ya Msingi Santhome Iliyopo Nkuhungu Dodoama kikiwa kimevalia mavazi nadhifu wakati ikiongoza wanafunzi wa Shule yao katika maandamano ya ufunguzi wa Wiki ya Elimu Hapa Nchini.
Sehemu ya Wanafunzi wa Shule mbali mbali za mkoani Dodoama wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa Wiki ya Elimu Hapa Nchini.
Mamia ya wanafunzi kutoka shule mbali mbali za Mkoa wa Dodoma waliandamana kuanzia Uwanja wa kumbu kumbu ya Mwl. Nyerere kupita Barabara ya Nyerere hadi Uwanja wa Jamhuri katika maadhimisho ya siku ya Elimu hapa Nchini.Uzinduzi ambao ulifanywa rasmi na Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda katika Uwanja wa Jamhuri na kuhudhuriwa na mawaziri na manaibu wa Wizara zinazo shughulika na Elimu pamoja na wadau wa Elimu hapa Nchini.
Picha na Deusdedit Moshi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati Dodoma.
No comments:
Post a Comment