Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwashi Ngehu(38) Mkazi wa Kijiji cha Chamalendi Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amefariki Dunia kwa kujinyonga kwa kutumia khanga baada ya kupatwa na hasira ya kufiwa na mtpto wake wa Kike
Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo lilitokea hapo jana majira ya saa kumi na moja alifajiri Kijijni hapo
Katika tukio hilo ni kwamba marehemu marehemu alikuwa akimuuguza mwanae wa kike kwa muda wa miezi miwili ambae alikuwa ni mtoto pekee wa marehe huyo
Alisema ndipo hapo juzi mwae huyo alifariki dunia na kuzikwa kijijini hapo na muda wote wa msiba marehemu alikuwa akilia kwa uchungu kufiwa na mwanae huyo wa pekee
Kidavashari alieleza marehemu alikuwa akiwaeleza waombolezaji waliofika kufariji msibani kuwa amepatwa na uchungu sana kufiwa na mtoto wake ambae alimzaa kwa shida sana kwani waliishi na mume wake kwa muda mrefu bila kujaliwa kupata mtoto
Alisema marehemu alikuwa akiwaeleza waombolezaji kuwa haoni faida ya kuishi tena Dunia bila kuwa na mtoto yoyote yule
Alieleza ndipo hapo juzi majira ya usiku wakati alipokuwa amelala ndani ya nyumba yake alipotoka nje na kuwaaga ndugu zake waliokuwapo msibani hapo kuwa anatoka nje kwenda kujisaidia
Alisema marehemu hakurejea tena ndani ya nyumba hadi hapo juzi majira ya saa kumi na moja mwili wake ulipokutwa ukiwa unang’inia juu ya mti huku akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia khanga yake
Mwili wa marehemu umeisha fanyiwa uchunguzi wa Kidakitari na wamekabidhiwa ndugu zake kwa ajiri ya mazishi ambayo yalifanyika hapo jana kijini hapo

No comments:
Post a Comment