ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 18, 2014

ITV HABARI,KUHUSU BOMU LILILOTEGULIWA HUKO MTWARA


Jeshi la polisi na JWTZ wafanikiwa kuharibu bomu lililotelekezwa Mtwara.
 Jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kushirikiana na jeshi la wananchi wa Tanzania wamefanikiwa kuharibu  bomu lililokuwa limetelekezwa katika kijiji cha Mdui kata ya Mbawala wilaya ya Mtwara vijijini baada ya kuonekana likichezewa na watoto.
jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kushirikiana na jeshi la wananchi wa Tanzania wamefanikiwa kuharibu  mlipuko wa bomu katika kijiji cha Mdui kata ya Mbawala wilaya ya Mtwara vijijini baada ya kuonekana likichezewa na watoto.
Akizungumza na ITV kaimu kamanda wa
polisi mkoa wa Mtwara Maisha Maganga amesema taarifa hizo wamezipata kutoka kwa raia wema baada ya kuonekana likiwa eneo la makaburi.
Amesema baada ya kupata taarifa juu ya bomu hilo lenye kilo nne jeshi hilo lilichukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kuomba kikosi maalum cha kutegua mabomu kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania.
Amesema bomu hilo linaonyesha ni la siku nyingi mahali hapo na  liliachwa enzi za vita ya Msumbiji.

1 comment:

Anonymous said...

mbona huko mtwara liliteguliwa zanzibar liki uwa mtu?