ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 8, 2014

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2014; KUNDI C NI NAFASI YA MWISHO YA KIZAZI CHA DHAHABU CHA IVORY COAST

COLOMBIA wapo kundi moja na Ugiriki, Ivory Coast na Japan katika Kombe la Dunia.
BIN ZUBEIRY inaendelea kukuletea makala za mchambuzi na beki wa zamani wa England, Martin Keown hapa akichambua Kundi C.

Mkongwe: Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba anatarajiwa kuendelea kuwa tegemeo la mabao la Ivory Coast
Kundi C
Colombia
Ugiriki
Ivory Coast
Japan
Utabiri wa Keown;
1 Ivory Coast
2 Japan
3 Ugiriki
4 Colombia
Ratiba (Saa za Afrika Mashariki)
Jun 14        Colombia v Ugiriki     Saa 1:00 usiku Horizonte
Jun 15        
Ivory Coast v Japan   Saa 10:00 jioni Recife
Jun 19        
Colombia v Ivory Coast Saa 1:00 usiku Brasilia
Jun 19        
Japan v Ugiriki          Saa 7:00 usiku  Natal
Jun 24        
Japan v Colombia     Saa 5:00 usiku  Cuiaba
Jun 24       
 Ugiriki v Ivory Coast  Saa 5:00 usiku Fortaleza
COLOMBIA
Viwango vya FIFA: Namba 8
Kocha: Jose Pekerman. Alisema kufuzu kwenda Brazil ilikuwa; "Moja ya furaha kubwa maishani mwangu". Muargentina huyo anafahamu cha kuzungumza katika nchi yake ya kuhamia.
Nahodha: Mario Yepes (Atalanta)
Mchezaji wa kumulikwa: James Rodriguez (Monaco) Radamel Falcao atakuwa nje, lakini mchezaji mwenzake wa Monaco atakuwa moja ya vipaji adimu nchini Brazil. Ufundi, uimara wake na kasi, vinamfanya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 asubiriwe kwa hamu watu waone vitu vyake katika Kombe la Dunia.
It's good to talk: Colombia captain Mario Yepes talks to reporters as the South Americans prepare for Brazil
Mazungumzo mazuri: Nahodha wa Colombia, Mario Yepes akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa maandalizi ya timu hiyo ya Amerika Kusini kwenda Brazil

Ubora wao: Kucheza pembezoni mwa Uwanja. Wakiwa na mawinga wawili wenye kasi na mabeki wawili wa pembeni hodari, Colombia wanapenda kuuteka mchezo.
Hatari: Hawafiki mbali. Colombia wamewahi kusonga mbele kutoka kwenye kundi lao mara moja t.
Watakwenda England? Arsenal imekuwa ikiwafuatilia kips wa Nice, David Ospina, Everton inampenda mshambuliaji wa Sevilla, Carlos Bacca na Newcastle imempa ofa kiungo wa Cagliari, Victor Ibarbo.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: 16 Bora (1990)
Walivyofika hapa: Walishika nafasi ya pili katika kundi gumu la Amerika Kusini kwa rekodi bora ya safu ya ulinzi kwenye bara hilo. 
Je, wajua? Kutakuwa na makocha watatu Wacolombia kazini katika Kombe la Dunia, lakini hakuna hats mmoja atakuwa anaifundisha timu yake ya taifa ya Colombia. Jorge Pinto (Costa Rica), Luis Fernando Suarez (Honduras) na Reinaldo Rueda (Ecuador) wote watakuwepo Brazil.
UGIRIKI   
Viwango vya FIFA: Namba 12
Kocha: Fernando Santos. Alishinda tuzo ya kocha bora wa muongo wa Ligi Kuu ya Ugiriki mwaka 2010, hivyo anajua anachokifanya.
Nahodha: Giorgos Karagounis (Fulham)
Mchezaji wa kumulikwa: Kostas Mitroglou (Fulham) japokuwa bado hajawakuna mashabiki wa Fulham baada ya kushindwa kuonyesha cheche tangu asajiliwa Januari, lakini mshambuliaji huyo alikuwa tegemeo na mfungaji bora wa Ugiriki katika mechi za kufuzu.
Great expectations: Greece fans have high hopes for Kostas Mitroglou despite his disappointing run at Fulham
Matarajio makubwa: Mashabiki wa Ugiriki wan a matumaini makubwa na Kostas Mitroglou licha ya kutokuwa na mwanzo mzuri Fulham

Ubora wao: Wamekaza buti. tarajia mbinu zile zile za wakati wanashinda Euro 2004 – ulinzi imara, kujituma na kufunga mabao.
Hatari: Kuteka hisia za mashabiki 
Watakwenda England? Beki wa Olympiakos, Kostas Minolas amekuwa akimulikwa na klabu za Ligi Kuu England kama Tottenham misimu ya karibuni. Georgios Samaras anatakiwa na Hull City.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Hatua ya makundi (1994 na 2010)
Walivyofika hapa: Walimaliza na point saws na Bosnia & Herzegovina katika Kundi D, lakini wakiwa nyuma yao kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa. Waliifunga Romania 4-2 jumla katika mechi ya mchujo kufuzu.
Mfungaji bora mechi za kufuzu: Kostas Mitroglou (Fulham)  mabao 5
Je, wajua? Baada ya kustaafu kama mchezaji akiwa na umri wa miaka 21, kocha Santos alikwenda kuchukua Shahada ya Umeme na Uhandisi wa Mawasiliano kabla ya kurejea kwenye soka miaka 12 baadaye. 
JAPAN 
Viwango vya FIFA: Namba 46
Kocha: Alberto Zaccheroni. Ukocha wa Japan ni kazi ya 14 kwa Mtaliano huyo, lakini ya kwanza katika soka ya kimataifa. 
Nahodha: Makoto Hasebe (Nuremburg)
Mchezaji wa kumulikwa: Keisuke Honda (AC Milan). Napenda kuwatazama Yasuhito Endo na Makoto Hasebe, lakini Honda ni Rolls Royce la Japan. Alianza 2010 na uwezo wake mkubwa na kutoa pasi za nipe nikupe vimemfanya awe mbunfu tegemeo la Japan.
Ubora wao: Kasi, soka ya kitaalamu. Wajapan wake vizuri katika kumiliki mpira na wan a viungo weledi wa uchezeshaji, ambao wamekuwa wakizivunja safu za timu pinzani. wanapiga pasi fupi, lakini wanashambulia kwa kasi.
Bright spark: Japan's Shinji Kagawa (centre) in action during this week's friendly win over Costa Rica
Mkali: Kiungo wa Japan, Shinji Kagawa (katikati) alicheza mechi ya kirafiki wiki hii dhidi ya Costa Rica

Hatari: Kuzuia. Katika mechi ya Kombe la Mabara niliwaona wametawala mchezo dhidi ya Italia, lakini wakaruhusu nyavu zao kutikiswa mara nne wakifungwa 4-3. Hilo ndilo shaka pekee kwao.
Watakwenda England? Atsuto Achida wa Schalke ni beki hodari wa kulia, ambaye Arsenal wamekuwa wakimmezea mate miezi ya karibuni. Aston Villa wanampenda kiungo mshambuliaji Hiroshi Kiyotake wa Nuremberg.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: 16 Bora (2002 na 2010)
Walivyofika hapa: Walifuzu kiulaini kileleni mea Kundi B kutoka Bara la Asia, wakiizidi kwa pointi nne Australia walioshika nafasi ya pili. 
Je, wajua? Japan imekuwa timu ya kwanza kufuzu katika kila fainali kati ya fainali tatu zilizopita za Kombe la Dunia. Walijikatia tiketi ya BrazilJuni 2013, mwaka mmoja na siku nane kabla siku ya ufunguzi wa Fainali za mwaka huu. 
IVORY COAST
Viwango vya FIFA: Namba 23
Kocha: Sabri Lamouchi. Mfaransa huyo alitumia muda kusoma mbinu za ufundishaji wa soka wa Mreno Jose Mourinho.
Nahodha: Didier Drogba (Galatasaray)
Mchezaji wa kumulikwa: Gervinho (Roma) Yaya Toure nfiye nyota wao, lakini Gervinho anaweza kutustaajabisha. Aliporomoka alipokuwa Arsenal, lakini msimu huu alikuwa mchezaji tofauti kabisa akiisaidia Roma kushika nafasi ya pili  Serie A. 
Ubora wao: Wanaijua soka. Wana uzoefu wa kutosha, lakini hii itakuwa nafasi ya mwisho kwa kizazi hike cha dhahabu kuacha kumbukumbu zao kwenye Kombe la Dunia.
Hatari: Ukuta uchochoro. Safu za kiungo na ushambuliaji ziko vizuri mno, tatizo kule nyuma, Kolo Toure na Didier Zokora wanaocheza kama mabeki pacha wa kati ni 'ugonjwa wa moyo'.
Watakwenda England? Kufanya vizuri kwa Seydou Doumbia wa CSKA Moscow kumewavutia Spurs na Chelsea. Didier Ya Konan wa Hannover anazivutia klabu za England sawa na Salomon Kalou.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Hatua ya makundi (2006 na 2010)
Walivyofika haps: Walifuzu kiulaini wakiongoza Kundi C na kuifunga Senegal mabao 4-2 jumla katika mechi maalum ya mchujo kuwania kufuzu. 
Je, wajua? Hizi zitakuwa fainali za kwanza za Kombe la Dunia kwa Lamouchi. Mfaransa alikuwemo kwenye kikosi cha awali cha timu yake ya tiara kabla ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1998 nyumbani kwao, lakini akaenguliwa na kuwashuhudia wachezaji wenzake wakitwaa Kombe.
Via Bongo Starz

No comments: