Ni miaka miwili tangu ututoke asubuhi ya Juni 18,saa mbili asubuhi mpendwa wetu Dommy. Hatuwezi kamwe kusahau ucheshi, upendo na moyo wako wa ushujaa uliokuwa nao wakati wa uzima wa afya pamoja na kipindi kigumu cha kuugua. Unakumbukwa sana na Mke wako Bernadeta watoto KageBriana, Bryan Mwombeki na Bryton Richard. Kwa namna ya kipekee tunapenda kuzidi kutoa shukrani zetu za zati kwa watanzania wa DMV chini ya Raisi Iddi Sandale, Mwakilishi wa familia yetu,Mama Salma Moshi Mama (Nyoka), Jumuiya mbalimbali Marekani, watanzania, ndugu, jamaa na marafiki wote kwa ujumla kwa msaada wenu wa Sala, michango mbalimbali ikiwa ni pamoja na ya kifedha, mawazo na ushauri wa kitaalamu na uuguzi. Shukrani pia ziwaendee wote waliotoa muda wao kumuuguza Dommy kulala Hospitali wakimuuguza, Dada Jessica Mukandala, Dada Salma Moshi,Dada Agness, Steven Msungu, Maburi Kahwa-Texas, nanyi wote mliotoka mbali kuja kumuuguza Dommy.Asanteni pia wachungaji na mapadre DMV, Padre Shao, wachungaji Shideko, Mbatta,Igogo,Kajoro,Malecela na wachungaji na mapadre wote waliomwongoza mpendwa wetu Dommy kiroho na hasa saa zake za mwisho kuondoka katika neema na usafi wa moyo. Daktari Seche Malecela, asante sana kwa mwongozo wako wa kitaalamu. Familia ya Mzee Kente, familia ya Mama Georgina Kaiza na bila kusahau mfuko wa Westadi chini ya Dada Rehema Chuma. Shukrani kwa vyombo vya habari hasa kwa timu nzima ya vijimambo chini ya Dj Luke na Radio Wapo chini ya Ndg. Anthony Magori, Sunday Shomari, Swahili Villa, Mubelwa Bandio na Issa Michuzi kwa msaada mkubwa wa kuhabarisha hasa wakati wa kipindi kigumu cha kuuguza na hatimaye kifo. Nafasi haitotosha kutoa shukrani kwa kila mmoja wenu ila tunaomba mpokee shukrani zetu za zati kabisa kutoka mioyoni mwetu. Asante kwa moyo wenu wa upendo mliouonyesha wakati familia yetu ilipokuwa na wakati mgumu katika kipindi cha safari ya mwisho ya mpendwa wetu Domitian Rutakyamirwa. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awazidishie maradufu.
Dommy hatuwezi kusahau maneno yako ya ujasiri na matumaini kwetu " Mwamini Mungu Yote yatakuwa"
Ni Sisi Bernadeta Kaiza, KageBriana,Bryan Mwombeki na Bryton Richard.
Bwana alitoa na akatwaa kilicho chake, Jina lake na libarikiwe.
Sleep on and on...

3 comments:
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe upumzike kwa amani, Amina
Kwa kweli ilikuwa ni uchungu kwa ndugu na jamaa tunawapa pole wote wazazi wa marehemu hasa Mama mzazi aliyeshuhudia kifo cha mtoto wake wakiwa pamoja na Dada wa marehemu kwa kweli kilikuwa kipindi kigumu sana kwao.
Mungu awatie nguvu hasa kupoteza mtoto akiwa kijana bado na ningependa kutoa pole kwa Berena na familia yake na Mtoto mpendwa wa marehemu aliyeko Tanzania.
R.I.P DOMITIAN
R.I.P Domitian, Mungu akulaze mahali pema peponi kwa kweli Marehemu alikuwa mcheshi kwa watu wote, Bernadetha umewasahau Mr and Mrs Pius Mutalemwa walifanikisha safari ya marehemu kwa kumkatia WESTADI kwa kweli Mungu awazidishie pale palipopungua kwani wametufungua watanzania wengi macho tulikuwa hatujaifahamu WESTADI.
Hapa duniani tunapita jamani tujaribu kupendana kwa dhati kama upendo tuliouonyesha wakati wa kuugua kwa Marehemu.
Nawashukuru sana wote tulioshiriki kumuuguza ndugu yetu tulijitahidi lakini MwenyeenziMUNGU alimwita hii ni njia ya wote kilamtu ataenda kwa ahadi yake nawashukuru sana kwa kuthamini mchango wangu niliweza kuwa mwakilishi wa familial Bila kujali natokea mkoa gani huu ni mfano wa kuigwa mwisho nakuombea MwenyeenziMUNGU akukinge na shari akupe nguvu na riziki uwatunze watoto na kumuomba MwenyeenziMUNGU amrehemu ndugu yetu na kuiweka roho yake mahala pema peponi Ameni
Post a Comment